SIASA

Balala ataka uchaguzi uwe baada ya miaka 10

Image result for BALALA WA KENYA
WAZIRI wa Utalii Kenya, Najib Balala amependekeza Uchaguzi Mkuu ufanyike kila baada ya miaka 10 ili kuepuka matatizo kwenye sekta ya utalii likiwemo la kupungua kwa watalii nchini humo kama ilivyo sasa.
“Ukiniuliza mimi ningependekeza kwamba tufanye uchaguzi baada ya miaka 10 angalau tusipate matatizo tunayoshuhudia sasa kwenye sekta ya utalii,” alisema Waziri Balala hivi karibuni wakati wa hafla ya usiku wa utalii. Alisema, idadi ya watalii wanaotoka nje ya nchi hiyo inatarajiwa kupungua kwenye miezi ya mwisho wa mwaka huu na kwamba, hali ya utalii nchini si nzuri sana.
Kati ya Januari hadi Juni mwaka huu idadi ya watalii iliongezeka kwa asilimia 10. Kwa mujibu wa Waziri Balala, ndege ndogo za kukodi zinakwenda pwani ya nchi hiyo bila abiria na kuna sehemu za kutalii hazina wageni kabisa. Alitaja baadhi ya maeneo yaliyoathirika kuwa ni Mombasa, Malindi na ranchi ya Ol Pajeta, Laikipia inayoaminika kuwa ni eneo kubwa zaidi linalotunza wanyama Afrika Mashariki. Kwa mujibu wa kiongozi huyo, hali ya siasa nchini humo inaziathiri sana hoteli na maeneo yenye wanyama kwa kuwa watalii wanasubiri kuona mambo yatakuwaje.
Alitoa mfano kuwa, kati ya Aprili na Agosti mwaka huu, idadi ya wageni watalii iliongezeka hadi 300,000 kutoka 245,000 ya mwaka jana kwa sababu ya kuhama kwa nyumbu, lakini idadi imepungua na watalii kutoka nje wataacha kwenda nchini humo. Alisema, hofu ya watoa wadau sekta ya utalii ina mantiki kwa sababu hata idadi ya watalii wa ndani imepungua kulinganisha na miaka miwili iliyopita.
Mwaka huu Kenya ilitarajiwa kupata watalii milioni 1.4 kwa ajili ya biashara na kupumzika. Watalii 937,000 kati ya waliokwenda Kenya mwaka jana walikwenda likizo, 78,000 walikwenda kwa sababu za kibiashara, wengine 136,000 kwa sababu nyingine.
Mwaka 2016 wageni milioni 3.6 walilala kwenye hoteli za Kenya, mwaka 2015 walikuwa milioni 3.1 hivyo kulikuwa na ongezeko la asilimia 14.6. Asilimia 35 ya watalii wa Kenya wanatoka Ulaya, asilimia 29 wanatoka Afrika, 17 Asia na 14 wanatoka Marekani. Mwaka 2016 sekta ya utalii Kenya ilipatia Sh bilioni 99.7 za Kenya, mwaka 2015 nchi hiyo ilipata wageni milioni 1.1 zikapatikana Sh bilioni 84.6 za Kenya.

 Polisi wavunja maandamano ya upinzani Kenya.

Image result for strike in kenya election
Polisi nchini Kenya wametumia rungu na gesi ya kutoa machozi kuvunja maandamano katika makao makuu ya tume ya uchaguzi IEBC mjini Nairobi.
Polisi wavunja maandamano ya upinzani Kenya
Waandamanaji wamekuwa wakitaka kufutwa na kuchukuliwa hatua za kisheria maafisa wa vyeo vya juu wa IEBC, kufuatia kufutwa kwa uchaguzi wa urais mwezi uliopita wakidai kuwa maafisa hao walimpendelea Rais Uhuru Kenyatta.


Makosa ya tume ya uchaguzi Kenya yafichuliwa.


SUPREME COURT JUDGES
Mahakama ya juu inaendelea kutoa sababu za kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi wa urais nchini Kenya kufuatia hatua ya upinzani kwenda mahakamani kupinga matokeo hayo.






''IEBC inafaa kufanya maandalizi mapya''


Jaji mkuu nchini Kenya David Maraga amefanikisha uamuzi wa mahakama kuu kuhusu kufutiliwa mbali kwa matokeo ya urais.
''Mfumo wa uchaguzi nchini Kenya ulitengezwa kuwa rahisi na wenye uhakika''. ''Kati ya tarehe 8 na 11 mwezi Agosti uchaguzi uliofanywa haukuwa hivyo'' alisema.
''Kesi ya kupinga uchaguzi iliopo mbele yetu ilikuwa rahisi kuelewa''.
''Ni wazi kwamba IEBC haikuelewa. IEBC inafaa kurudi katika maandalizi yake'' , jaji Maraga aliongezea.
''Mahakama nyengine pia ingefanya uamuzi kama huu iwapo makosa yaliofanyika katika uchaguzi yatarejelewa'', aliongezea.
Image result for jaji mkuu kenya





''Uchaguzi haukuwa na uwazi wala haukuhakikiwa''


Mahakama ya juu nchini Kenya imesema kuwa ilifutilia mbali uchaguzi wa urais nchini humo kwa sababu haukuwa na uwazi wala ithibati .
Mahakama hiyo imelaumu tume ya uchaguzi ya IEBC na mwenyekiti wake kwa kushindwa kupokea matokeo yote kabla ya kutangaza matokeo ya urais.
Pia imekosoa tume hiyo ya uchaguzi kwa kukaidi amri ya mahakama kufungua sava za kompyuta zake ili zichunguzwe hatua iliofanya mahakama hiyo kukubali madai ya upinzani kwamba mfumo wa kutangaza matokeo ulikuwa umeingiliwa na kutumiwa vibaya.






0 comments:

Post a Comment

Search This Blog

  • ()
Powered by Blogger.

Yaliyojiri leo

Tanzania yaanza majaribio dawa kinga ya Ukimwi

LIKE OUR FACEBOOK PAGE

Contact us

Name

Email *

Message *