Tanzania yaanza majaribio dawa kinga ya Ukimwi


Dar es Salaam. Serikali imesema tayari nchi imeanza rasmi majaribio ya dawa kinga mpya inayozuia maambukizi ya virusi vya Ukimwi (PrEP), huku ikikanusha kuwapo kwa dawa inayotibu ugonjwa huo.

Dawa kinga hiyo mpya ina uwezo wa kuzuia maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) ikiwa mtumiaji atameza kila siku kwa muda wa siku saba kabla hajashiriki tendo la kujamiiana, ataendelea kumeza kwa kipindi chote atakachokuwa katika hatari ya kuambukizwa.

Hayo yamesemwa leo Mei 9, 2018 mjini Dodoma na naibu waziri wa Afya, Dk Faustine Ndugulile wakati wa uzinduzi wa mpango wa nne wa VVU na Ukimwi katika sekta ya afya (HSHSP IV 2017-2022) sambamba na maadhimisho ya miaka 30 ya Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Ukimwi.

Amesema taarifa kwamba nchi inazindua tiba dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi, si sahihi kwani Tanzania haijapata tiba hiyo.

"Kinachoendelea tumezindua dawa kinga, kuna dawa ambayo tunataka tuielekeze katika makundi ambayo tunayaona yapo kwenye hatari ya kuambukizwa virusi vya Ukimwi, watapatiwa kwa lengo la kuwakinga wasipate,” amesema Dk Ndugulile na kuongeza:

“ila sio suluhisho na tuseme vilevile kwamba hatujapata tiba ya virusi vya Ukimwi na utaratibu huu wa dawa kinga, ndiyo inaanza majaribio sasa na haijaanza kupatikana.”

Dawa hizo mpya zenye uwezo wa kukinga maambukizi dhidi ya VVU kwa asilimia 99, zilizoanza kutumika katika baadhi ya nchi za Kusini mwa Afrika, zinakuja wakati ukanda huo ukiongoza duniani kwa kuwa na asilimia 50 ya waathirika wote duniani.

Utafiti uliofanywa na mwanasayansi kutoka Chuo Kikuu cha London, Dk Sheena McCormack umeonyesha kuwa PrEP inazuia maambukizi ya Ukimwi kwa kuua virusi baada ya kufanyiwa majaribio na kundi la wapenzi wa jinsia moja, ambao wamo katika hatari zaidi ya maambukizi.
Shirika la Afya Duniani (WHO) limetambua kwamba dawa hiyo ya tembe inaweza kupunguza maambukizi kwa kiwango kikubwa.

Share:

Bukoba: Baba mzazi awachinja wanawe mapacha na kuwatenganisha vichwa na viwiliwili kisa ugomvi na mkewe

Image result for killing by using knives

Kuna jamaa amechinja watoto wake mapacha wenye umri wa miaka saba huko Bulambizi kata Kanyangereko jimbo la Bukoba vijijini mkoani Kagera.Kila mtoto kichwa kimetenganishwa na kiwiliwili.Inasemekana ni wivu wa kimapenzi.

Kama walivyozaliwa wawili kwa pamoja, ndivyo walivyofariki dunia.
Ni watoto pacha wenye umri kati ya miaka minne na mitano, Nyakato (mvulana) na Nyangoma (msichana) wa Kijiji cha Butahyaibeba wilayani Bukoba waliouawa kwa kuchinjwa na mtu anayedhaniwa kuwa baba yao mzazi usiku wa kuamkia jana.

Kwa mujibu wa Dickson Barongo, mwenyekiti wa kitongoji cha Bulambizi ambako mauaji hayo yametokea, watoto hao walichinjwa na kutenganishwa vichwa na viwiliwili.

“Nilikuwa wa kwanza kufika eneo la tukio baada ya kufuatwa nyumbani na mtoto aliyenusurika,” alisema Barongo.

Hata hivyo, alisema mama wa watoto hao alikimbia wakati mume wake akifanya tukio hilo ili kujinusuru.

Barongo alisema kabla ya kufanya mauaji hayo, mzazi huyo aliwachukua watoto hao na kuwafungia chumbani.

“Chanzo cha mauaji hayo kinahusishwa na ugomvi kati ya wanandoa hao,” alisema.

Inadaiwa kuwa baada ya wanandoa hao kutengana, mwanamke alienda kuishi kwao akiwaacha watoto na baba yao.

“Lakini juzi alifika hapo kwa mume wake akawaomba wakamtembelee Alhamisi ya wiki iliyopita na jana (Jumamosi) alikuwa amewarudisha kwa baba yao,” alisema.

“Mume alimruhusu mzazi mwenzake kuondoka na watoto hao na siku ya tukio alikuwa amewarejesha kwa baba yao lakini baba alimzuia mke wake kuondoka na akafunga mlango, lakini wakati wa vurugu hizo alifanikiwa kutoroka,” alisema.

Barongo aliongeza kuwa walimpata mtuhumiwa kwa njia ya simu na akawajibu kuwa bado hajamaliza kazi na baadaye simu yake haikupatikana.

Msimamizi wa zamu katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera, Gloria Mpango alisema uchunguzi wa awali unaonyesha watoto hao walichinjwa na kutenganishwa vichwa na viwiliwili na wanasubiri taratibu za polisi kabla ya ndugu kuruhusiwa kuchukua miili kwa mazishi.
Share:

BREAKING NEWS!! FORM FOUR RESULTS OUT!!!!




By Eliud Adson.

Dar es Salaam. Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) limetangaza matokeo ya kidato nne ambapo ufaulu umeongezeka kwa asilimia saba.

Jumla ya watahiniwa 385, 767 walisailiwa kufanya mtihani kidato cha nne mwaka 2017, kati yao 287,713 sawa na asilimia 77.09 ndio wamefaulu ambapo wasichana ni 143,728 sawa na asilimia 75.21 na wavulana 143,985 sawa na asilimia 79.06.

Akitangaza matokeo hayo leo Januari 30, 2018 Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde amesema mwaka 2016 watahiniwa waliofaulu walikuwa 277,283 sawa na asilimia 70.09.

Amesema matokeo ya watahiniwa 50 wa shule ambao walipata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya baadhi ya masomo ya mitihani hiyo, watapata fursa hiyo mwaka huu.
"Watahiniwa 77 wa shule ambao walipata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya mtihani watapata fursa mwaka 2018," amesema Dk Msonde.

Dk Msonde amesema watahiniwa 265 waliobainika kufanya udanganyifu katika mitihani matokeo yao yamefutwa huku mtahiniwa mmoja akiandika matusi katika karatasi yake ya majibu.

BONYEZA HAPA KUYAPATA MATOKEO
Share:

ELIZAYO HB KAJA KIVINGINE ANAKWAMBIA BYE BYE, PAKUA HAPA KUUPATA WIMBO WAKE MPYA

New Hit song from Elizayo unique

ELIZAYO UNIQUE_-_BYE BYE_PRODUCED_BY_CHUMA&MR.T TOUCH_FREE_NATION_.mp3 DOWNLOAD
Share:

Chadema mguu nje, ndani uchaguzi Kinondoni, Siha



Dar es Salaam. Chadema, ambayo pamoja na vyama vingine vitano vilisusia uchaguzi mdogo katika majimbo matatu, sasa ipo njiapanda kusimamisha wagombea katika majimbo ya Kinondoni na Siha.

Wakati bado hakijatangaza kubadili msimamo huo, uongozi wa ngazi ya Wilaya ya Kinondoni umeanza kutoa fomu kwa ajili ya mchakato wa kupata mgombea kwa maelezo kuwa umeruhusiwa na uongozi wa juu wa chama hicho kikuu cha upinzani.

Lakini uongozi huo wa juu umesema bado haujafanya uamuzi kuhusu kushiriki uchaguzi katika majimbo hayo uliopangwa kufanyika Februari 17 na msimamo huo unaweza kutolewa wakati wowote, Mwananchi imeambiwa.

Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Itifaki wa Chadema, John Mrema alisema jana kuwa wameunda kamati ndogo inayofanya utafiti kuhusu mchakato huo na kwamba uchukuaji fomu huo bado haujapewa baraka za ngazi za juu.

“Hatuna uamuzi wowote hadi sasa, ingawa ule wa awali wa kutoshiriki bado upo,” alisema Mrema.
“Lakini leo uamuzi utatoka. Bado tupo katika mjadala.”

Majimbo hayo mawili yanarudia uchaguzi baada ya waliokuwa wanayashikilia Maulid Mtulia (CUF, Kinondoni) na Dk Godwin Mollel (Chadema, Siha), kujiuzulu nafasi zao kwa nyakati tofauti na kuhamia CCM mwezi uliopita.

Mtulia alitangaza kujiuzulu ubunge Desemba 2 mwaka jana akisema hakushawishiwa na mtu yeyote, bali amebaini kuwa Serikali ya CCM inafanya kazi kubwa ya kutekeleza ilani yake na inafanya vizuri katika mambo mengi ambayo upinzani uliahidi kuyatekeleza.

Wakati Mrema akisema bado wanajadili ushiriki wa Chadema, uongozi wa Wilaya ya Kinondoni umeshaanza mchakato wa kupata mgombea wa kumrithi Mtulia ambaye mwaka 2015 alisimamishwa na vyama vinne vilivyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kutokana na makubaliano maalumu.

Uongozi huo umesema utasimamisha mgombea atakayepambana na Mtulia aliyepitishwa na CCM kuwania tena kiti hicho.

Mwenyekiti wa Chadema wa Kinondoni, Waziri Muhunzi aliiambia Mwananchi jana kuwa baada ya kutafakari kwa kina na kuona mwenendo katika uchaguzi uliopita wa marudio katika majimbo matatu, wameamua kuanza mchakato wa kumsimamisha mgombea.

“Chadema wilayani Kinondoni, ndio tulioamua kuuomba uongozi wa juu kusimamisha mgombea wa jimbo hili na tuna imani litarudi mikononi mwa Ukawa,” alisema.

“Ingawa jambo hili halikuwa rahisi, nawashukuru viongozi wa juu kwa kutuelewa na kuturuhusu.
“Ugumu ulikuwapo kutokana na msimamo wa viongozi wa juu kuhusu malalamiko yao waliyoyatoa huko nyuma kuhusu uchaguzi wa kata 43. Hata hivyo, uchaguzi wa majimbo matatu tumeona baadhi ya mambo yameanza kufanyiwa kazi ikiwamo polisi kutoingilia.”

Muhunzi alisema uchaguzi huo ni kipimo kwao cha kuangalia yale malalamiko dhidi ya wakuu wa wilaya kuingilia uchaguzi yatajitokeza tena kwa kuwa kwenye uchaguzi wa majimbo matatu uliofanyika hivi karibuni hayakujitokeza.

Alisema tayari wanachama 11 wamejitokeza kuomba nafasi ya kugombea ubunge wa jimbo hilo kati yao ni madiwani wanne.

“Mwisho wa kuchukua barua za kutangaza nia ya kuomba kugombea ni leo saa 10:00 jioni. Baada ya hapo kamati ya utendaji itakutana kwa ajili kutoa utaratibu wa kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa kugombea jimbo hili.

“Thamani ya fomu ni Sh 250,000 ambazo watangaza nia hao watazichukua na kujaza kisha kuzirudisha kwa hatua nyingine zaidi,” alisema Muhunzi.

Muhunzi aliwataja wanachama waliojitokeza kutangaza nia kuwa ni Juma Uloleulole (diwani Kijitonyama), Agrey Nicolaus, Elisante Emmanuel, Moza Ally, Francis Nyerere, Rose Moshi (diwani viti maalumu), Ray Kimbita (diwani Hananasif) na Mustafa Muro (diwani Kinondoni). Boniface Obedi, Shabaan Moyo na David Assey.

Kuhusu Ukawa, Muhunzi alisema endapo CUF upande wa Maalim Seif Sharif Hamad ungemsimamisha mgombea, Chadema ingeheshimu uamuzi huo kama ilivyokuwa katika Uchaguzi Mkuu wa 2015.

“Kutokana na mgogoro unaondelea ndani ya CUF, tumesikia upande ule wa Profesa Ibrahim Lipumba unasimamisha mgombea, hivyo hatuwezi kuwaachia bora ingekuwa Maalim Seif,” alisema Mahunzi.

Katibu wa Chadema Mkoa wa Dar es Salaam, Henry Kilewo alisema kura za maoni zinatarajiwa kufanyika leo na kwamba mchakato wa kukagua ujazaji wa fomu za kuomba ulikamilika jana.
Kwa upande wa Siha, kaimu mwenyekiti wa Chadema wa Kilimanjaro, Joseph Selasini alisema bado wanasubiri maelekezo ya Kamati Kuu ya chama hicho.

Hali kama hiyo ilijitokeza mkoani Singida ambako uongozi wa mkoa ulisimamisha mgombea jimbo la Singida Kaskazini, lakini viongozi wa taifa wakaagiza aliyepitishwa kugombea ajitoe kuheshimu msimamo wa chama hicho.
Share:

HESLB Yatangaza majina ya taasisi 57 zisizopeleka makato ya wanaufaika wa mikopo kwa wakati

MIKOPO-HESLB.png
Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) imeanika majina 57 ya kampuni, shule, vyuo na mashirika ambayo waajiri wake hawawasilishi makato ya wanufaika wa mikopo kwa wakati.

Uanikaji wa majina hayo kupitia tovuti ya HESLB umekuja siku mbili baada ya kutangaza kufanya hivyo Jumatano iliyopita.
Mkurugenzi Msaidizi Urejeshaji Mikopo, Phidelis Joseph alisema kabla ya kuanza kuwasaka wanufaika 119,497 ambao hawajarejesha mikopo yao, wataanika majina yao hadharani.

Miongoni mwa kampuni zilizotajwa ni pamoja na Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI), Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (Dawasco), Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Shirika la NSSF, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Puma Energy Limited, Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), Bohari Kuu ya Dawa (MSD) na Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC).

Zipo pia shule za sekondari ambazo waajiri wake hawapeleki fedha kwa wakati licha ya kuwakata wafanyakazi wao.

Akifafanua kuhusu muda wa kuwasilisha fedha za makato ya wanufaika, Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul-Razaq Badru alisema kila mwajiri ana wajibu wa kisheria wa kuwasilisha makato ya wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu kwa Bodi ndani ya siku 15 baada ya mwisho wa mwezi.

“Baadhi ya waajiri wamekuwa hawafanyi hivyo na kuilazimisha Bodi ya Mikopo kuanza kuwasaka kwa nguvu.

“Katika msako huu hatutamuacha mtu au mwajiri yeyote anayekiuka sheria iliyoanzisha Bodi,” alisema Badru.

Kaimu Mkurugenzi wa Habariwa HESLB, Omega Ngole alisema kwamba idadi ya wanaokwenda kulipa madeni yao imeongezeka.

Alisema kwa kawaida ofisi zao za kanda zilizopo Arusha, Dodoma, Mwanza na Zanzibar hupokea wadaiwa wapya kati ya 15 hadi 25 kwa siku, lakini kuanzia jana wamepokea zaidi ya 50.

Akizungumzia zaidi kuhusu ofisi za makao makuu, Ngole alisema: “Tunapokea wadaiwa wapya wanaotaka kulipa zaidi ya 300 ambayo haikuwa kawaida, wapo na viongozi ambao majina yao yapo kwenye orodha ya wadaiwa, wamemaliza leo.”

Alisema kwamba wanawashukuru wote kwa kutimiza wajibu wao kwa kuwa fedha hizo zitatumika kwa ajili ya kuwasomesha wahitaji wengine.
Share:

LIONEL MESS KUONDOKA BARCELONA FC

Baba mzazi wa nyota wa Barcelona Lionel Messi, Jorge Messi amesema, taarifa zinazosamba kuwa endapo jimbo la Catalonia litajitenga kutoka Hispania nyota huyo ataachana na klabu hiyo kuwa ni uongo.
Jorge ambaye pia ni wakala wa mfungaji huyo ameyasema hayo kwenye mahojiano na 'Radio Red' ya Argentina na kufafanua kuwa hakuna kipengele kinachotaka Messi aondoke Barcelona endapo Catalonia itajitenga na Hispania
''Taarifa hizo ni za uongo, mkataba mpya wa Messi hauna kipengele hicho, ila tu kuna maelewano yanayotaka pande zote mbili kuzingatia kuwa Barcelona ni timu kubwa na inawachezaji wakubwa kwahiyo inatakiwa kucheza ligi kubwa haijalishi ni ligi gani ila iwe moja ya ligi kubwa'', amesema Jorge.
Messi ambaye pia ni mfungaji bora wa muda wote wa Argentina mwezi Novemba mwaka jana alisaini mkataba mpya wa kusalia Camp Nou mpaka mwaka 2021 huku gharama ya kuuzwa ikiwekwa kuwa ni € 700 milioni ambazo ni takribani shilingi  bilioni 2.
Msimu huu Messi ana mabao 15 kwenye LaLiga, huku Barcelona ikiwa pointi 45, tisa juu ya Atletico Madrid inayoshika nafasi ya pili ikiwa 36.

Share:

Dkt. Shika kuiaga Tanzania mazima

Dkt. Louis Shika ambaye amejipatia umaarufu baada ya kutangaza dau la kununua nyumba za Lugumi, amesema kwamba hivi karibuni anatarajia kwenda kusihi Marekani, baada ya Umoja wa Mataifa kumpandisha cheo.

Akizungumza kwenye kipindi cha Weekend Breakfast cha East Africa Radio, Dkt. Shika amesema awali alikuwa anafanya kazi kwenye shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia wakimbizi (UNHCR) na sasa amepandishwa cheo, hivyo hata ofisi zake hazitakuwa tena Nairobi nchini Kenya, kwani zitahamishiwa New York Marekani.
"Sasa hivi nina mpango wa kusajili kampuni yangu alafu mimi nisepe, nikiwa hapa nchini nanyanyasika, nilikuwa nafanya kazi na Umoja wa Mataifa  Bara la Afrika, sasa ni world wide ofisi itakuwa New York, nimepandishwa cheo, nafaya kazi ofisi ya UNHCR, hata mama Kevela alipogundua mimi ni balozi akasema nyinyi ndio mnaoongoza nchi hii, na watu wajue kuwa uteuzi wangu haukutokea Tanzania, nimeteuliwa kwa veto power, veto power ziko tano kwenye umoja wa mataifa, jina langu lilikuwa projected na Urusi na mwenyewe Putin", amesema Dkt. Shika.
Dkt. Shika ameendelea kwa kusema kwamba kura ambazo alipata zilitosha kwa yeye kuwa balozi wa Umoja wa Mataifa, kwani nchi tatu zilikubali jina lake kupitishwa ikiwemo na Marekani.
Share:

Download hapa majina ya walimu waliopangiwa vituo vya kazi

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo ametangaza ajira mpya 3,033 za walimu wa shule mbalimbali nchini za msingi na Sekondari ambao watakwenda kujaza nafasi za walimu waliobainika kuwa na vyeti feki.
Image result for selemani jafo kutangaza ajira mpya za walimu
Jafo alisema kuwa majina ya walimu hao wapya 3,033 yatatangazwa leo na kupangiwa vituo vya kazi, walimu 266 watakuwa ni walimu wa shule za sekondari na Walimu 2,767 watakuwa walimu wa shule ya msingi.
Aidha Jafo amewataka walimu hao wapya ambao wamechaguliwa kuripoti kwa Wakurugenzi wa halmshauri husika ambazo watakuwa wamepangia kuanzia Disemba 27, 2018 hadi Januari 7, 2018. 
Mbali na hilo Selemani Jafo amewaagiza Wakurugenzi wa Halmashauri ambazio walimu hao wataripoti kuwapokea na kuzingatia taratibu na kanuni zote za utumishi wa Umma na baadaye kutoa taarifa ya kuripoti kwao.
Orodha ya Majina ya walimu waliopangiwa vituo.pdf  DOWNLOAD
Share:

Tazama Ratiba ya 16 bora katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya(UEFA)

Champions League draw: Chelsea face Barcelona, Tottenham to play Juventus

Image result for uefa icon
Chelsea have been drawn against Barcelona in the last 16 of the Champions League, while Tottenham will face Italian champions Juventus.
Premier League leaders Manchester City will play Switzerland's Basel, Manchester United face La Liga side Sevilla and Liverpool take on Portugal's Porto.
Holders Real Madrid will face Paris St-Germain.
A record five English teams progressed from the group stage this season.
Chelsea were the only English team to make it through as runners-up, with the other four sides all topping their respective groups.
The Blues have arguably been handed the most difficult tie, and it comes days after boss Antonio Conte conceded that their Premier League title defence was over following their defeat by West Ham, which left them 14 points adrift of Manchester City.
However, Chelsea did beat Barcelona in the semi-finals before lifting the Champions League trophy in 2012.
Real Madrid, who are aiming for a 13th title and third in a row, were given a tough draw against big-spending PSG after finishing behind Tottenham in Group H.
The group winners will be away in the round of 16 first legs on 13/14 and 20/21 February, and at home in the return matches on 6/7 and 13/14 March.
The final will take place in Kiev on 26 May.

Champions League last-16 draw

Juventus v Tottenham (13 February and 7 March)
Basel v Manchester City (13 February and 7 March)
Porto v Liverpool (14 February and 6 March)
Sevilla v Manchester United (21 February and 13 March)
Real Madrid v PSG (14 February and 6 March)
Shakhtar Donetsk v Roma (21 February and 13 March)
Chelsea v Barcelona (20 February and 14 March)
Bayern Munich v Besiktas (20 February and 14 March)
Share:

Ronaldo amtangazia vita Lionel Mess

  • Mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo amefikisha tuzo tano sawa na mpinzani wake Lionel Messi.

Cristiano Ronaldo amesema ataendeleza ‘vita’ na mpinzani wake mkubwa Lionel Messi katika mbio za kuwania tuzo za mchezaji bora wa dunia.

Ronaldo alitoa kauli hiyo muda mfupi, baada ya kushinda tuzo ya mchezaji bora akimshinda Messi. Mshambuliaji huyo wa Real Madrid imefikisha tuzo tano sawa na mpinzani wake.

Nafasi ya tatu ilichukuliwa na mshambuliaji wa Paris Saint Germain (PSG) Neymar. Tuzo hizo zinatolewa Ufaransa na kura zinapigwa na waandishi wa habari 173.

“Nitapambana naye (Messi), nitahakikisha nakuwa kwenye kiwango bora. Nitacheza vizuri kwa klabu na timu ya taifa,” alisema Ronaldo alipoulizwa kuhusu nafasi ya Messi.

Alisema ataendelea kulinda kipaji chake kwa manufaa ya Real Madrid na timu ya taifa ya Ureno kwa kucheza kwa kiwango bora.

“ Nina furaha. Hili ni tukio kubwa katika maisha yangu, napenda kutoa shukurani kwa wachezaji wenzangu wa Real Madrid, pia nawashukuru watu wote walionifikisha hapa,” alisema Ronaldo.

Wakati wa kutoa shukurani, Ronaldo alitania anataka kupata watoto saba. Nguli huyo ana watoto wanne aliozaa na wanawake watatu tofauti.

Nyota huyo alikwenda Paris na ndege binafsi akiongozana na familia yake.
Share:

Polisi, TCRA wazungumzia akaunti ya Mange Kimambi

Jeshi la Polisi limetaka liachwe liendelee kufanya kazi yake kwa weledi katika kushughulikia suala la Mtanzania aishiye ughaibuni, Mange Kimambi, ambaye anatuhumiwa kuchapisha taarifa zinazodaiwa kuwatusi mitandaoni watu mbalimbali wakiwamo viongozi.


 Akizungumza na Nipashe  kuhusiana na uwezekano wa wao kuifunga akaunti ya Kimambi ikiwa sehemu ya hatua wanazochukua kwa sasa, Msemaji wa Jeshi la Polisi, Barnabas Mwakalukwa, alisema ni kweli jeshi lao linalifanyia kazi suala hilo.
Hata hivyo Mwakalukwa hakutaka kukubali au kukataa juu ya kile kilichodaiwa kutokea kwenye akaunti ya Kikambi na badala yake kutaka apewe muda wa kulifanyia kazi ndipo alitolee maelezo ya kina.
Hili jambo lina mambo mengi sana. Watu wengi wanahusika na taasisi nyingi (pia) zitahusika kulishughulikia, Hivyo tunaendelea kupokea mawazo ya watu mbalimbali kuhusu namna ya kwenda nalo… mawazo wanayotupa tunayafanyia kazi lakini naomba mtuache kwanza tunaendelea kulishughulikia,” alisema Mwakalukwa.
Aidha wakati Msemaji wa Polisi akisema hayo, TCRA ilisema kuwa haiwezi kufunga wala kuingilia akaunti ya Kimambi kwa sababu huo siyo wajibu wake kisheria.
Msemaji wa TCRA, Semu Mwakyanjala, aliiambia Nipashe kuwa mamlaka yao haina nguvu za kisheria kufanya kazi hiyo bali wenye wajibu wa kufanya hivyo ni kitengo cha kudhibiti uhalifu wa mitandaoni cha Jeshi la Polisi.
Akifafanua zaidi, msemaji huyo alisema makosa yote yanayohusu mitandao, yakiwamo ya watu kutishiwa maisha, kutukanwa, kuibiwa kwa njia ya mtandao au kunyanyaswa kwa namna yoyote mtandaoni, wanaohusika ni polisi na siyo TCRA. 
Masuala ya akaunti za watu kwenye mitandao kama hiyo unayosema (ya Kimambi)… mwenye mamlaka ya kuingia na kuzifunga ni Jeshi la Polisi. Bunge liliipa mamlaka ya kisheria polisi kuchunguza na kukamata wahalifu kama hao… waulizeni wao,” alisema Mwakyanjala.
Hata hivyo zipo taarifa mitandaoni  zilimkariri Mtanzania huyo aishiye Marekani kuwa kilichotokea ni matokeo ya kazi ya wadukuzi wa mitandaoni, maarufu kama ‘hackers’ kupoteza akaunti yake yenye wafuasi takribani milioni 1.5.
Pamoja na hayo upo ujumbe wa lugha ya kigeni uliokuwa ukisambaa kwenye mtandao wa instagram ukionyesha kuwa akaunti inayofahamika kuwa ni ya Kimambi, imefungwa na waendeshaji wa mtandao wa Instagram kwa sababu ya kuwapo kwa malalamiko dhidi ya machapisho ya akaunti hiyo.
Share:

Search This Blog

  • ()
Powered by Blogger.

Yaliyojiri leo

Tanzania yaanza majaribio dawa kinga ya Ukimwi

LIKE OUR FACEBOOK PAGE

Contact us

Name

Email *

Message *