Basi linalojiendesha lapata ajali siku yake ya kwanza barabarani
Basi linalojiendesha huko Las Vegas lilihusika kwenye ajali wakati wa siku yake ya huduma.
Gari hilo lililokuwa limewabeba abiria kadha liligongwa na lori lililkuwa katika mwendo wa chini.
Hakuna mtu aliyejeruhiwa wakati wa ajali hiyo ambayo maafisa wanaema ilitokana na hitilafu ya dereva wa lori.
Basi hilo ndilo la kwanza la aina yake kutumiwa kwenye barabara za umma.
Ajali hiyo ilitokea siku moja baada ya Waymo - inayomilikiwa na kampuni ya Google, Alphabet, kutangaza kuwa inazindua teksi zinazojiendesha huko Phoenix, Arizona.
Basi hilo linawabeba hadi wau 15 na lina kasi ya hadi kilomita 45 kwa saa lakini kawaida mwendo wake ni kilomita 25 kwa saa.
Msemaji wa mji wa Las Vegas alisema kuwa ajali hiyo ilikuwa ni kidogo na kwamba basi hilo litarudi barabarani Alhamisi baada ya majaribio ya kawaida.
Lori la mizigo lilikuwa likitoka kupakia mizigo.
"Basi likafanya kile linastahili kufanya na kusimama. Kwa bahati mbaya dereva wa lori hakusimama, alisema afisa wa mawasiliano Jace Radke.
Ajali za magari yanayojiendesha zimeripotwa awali, lakini karibu ajali hizo zote zimesababishwa na makosa ya wanadamu.
Sasa imebainika kuwa idadi ya watu waliouawa katika mashambulio mawili ya mabomu mjini Mogadishu, Somalia, imepanda na kuwa zaidi ya 230.

Haijulikani nani alihusika, lakini kwa idadi ya maafa, hayo yalikuwa kati ya mashambulio makubwa kabisa nchini Somalia, tangu kundi la wapiganaji wa Kiislamu, al-Shabab, kuanza mapigano yao mwaka 2007.
Katika shambulio la kwanza, bomu lilokuwa kwenye lori, lililipuka kwenye njia panda, iitwayo Kilomita-5, ambapo kuna ofiisi za serikali, mahoteli na maduka, vyote viliporomoka katika mlipuko huo.
Saa mbili baadaye, bomu jengine lilikalipuka katika mtaa wa Medina.
Mkurugenzi wa Hospitali ya Madina, Mohamed Yusuf Hassan, anasema, alishtushwa na ukubwa wa shambulio hilo.
Lema atapoteza muda wake - Gambo
Mrisho Gambo amefunguka na kusema Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema anapaswa kutambua kuwa yeye kama Mkuu wa mkoa anajishughulisha na matatizo ya watu hivyo kama hatabadili aina ya siasa azifanyazo basi anapoteza muda wake kwa miaka mitano yote.

Gambo amesema kuwa yeye hana tatizo lolote na Mbunge huyo wa Arusha mjini na kudai kwamba anapaswa kutambua na kubadili aina ya siasa anazofanya kwa kuwa yeye amelenga kutatua matatizo na changamoto za watu wa Arusha Mjini.
"Msuguano na Mbunge haupo lakini anatakiwa tu asome alama za nyakati kwamba Mkuu wa Mkoa wa sasa amedhamiria kuhangaika na shida za watu kama hatalitambua hilo atapoteza muda wake kwa miaka yake yote mitano" alisema Mrisho Gambo
Aidha Mkuu wa Mkoa huyo amesema kuwa yeye kama kiongozi kijana anahitaji zaidi kukosolewa kuliko kusifiwa ili aweze kujirekebisha sehemu ambayo ana mapungufu ili aweze kuwa kiongozi madhubuti na mahiri zaidi.
0 comments:
Post a Comment