Korea Kaskazin Vs Marekani

Marekani yataka mataifa yote kukatiza uhusiano na Korea Kaskazini

Kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong un na mwenzake wa Marekani Donald Trump
Marekani imeyataka mataifa yote kukatiza uhusiano wa kidiplomasia na ule wa kibiashara na Korea Kaskazini baada ya taifa hilo kufanyia jaribio la kombora lake la masafa marefu.
Akizungumza katika baraza la usalama la umoja wa kimataifa ,mjumbe wa Marekani katika baraza hilo Nikki Haley amesema kuwa rais Trump amemtaka mwenzake wa China kukata usambazaji wa mafuta kwa Pyongyang.
Amesema kuwa Marekani haitaki mzozo lakini Korea Kaskazini itaangamizwa iwapo vita vitazuka.
Onyo hilo linajiri baada ya Pyonyang kufanyia majaribio kombora lake la kwanza katika kipindi cha miezi miwili.
Korea Kaskazini imesema kuwa kombora hilo lililorushwa siku ya Jumatano ambalo inasema liliruka kimo cha kilomita 4,475, ikiwa ni mara kumi zaidi ya kimo cha kituo cha angani.
Madai hayo hayakuthibitishwa na wataalam wametiliashaka uwezo wa taifa hilo kuwa na teknolojia kama hiyo.
Hatahivyo kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un amesema kuwa uzinduzi wa kombora hilo ulikuwa wa kufana.
Jaribio hilo likiwa mojawapo ya majaribio yaliofanywa na taifa hilo limeshutumiwa na jamii ya kimataifa na tayari baraza la usalama la umoja wa kimataifa limeitisha kikao cha dharura.
Bi Haley alionya kuwa kuendelea kwa uchokozi kunalenga kuliyumbisha eneo hilo.
''Tunahitaji China kuchukua hatua zaidi'', alisema.
Rais Trump alimpigia simu rais Xi Jinping mapema siku ya Jumatano , Ikulu ya Whitehouse ilisema kuwa rais Trump alizungumza na Xi Jinping kwa simu akimtaka kuchukua hatua zozote kuishawishi Korea Kaskazini kusitisha uchokozi na kusitisha mpango wake wa kinyuklia.
Bavicha yatoa salamu za kumuaga Katambi
Makamu Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema (BAVICHA), Patrick Ole Sosopi amesema kwamba kuondoka kwa Mwenyekiti wa baraza hilo Patrobas Katambi ndani ya Chama hicho hakijawateteresha na kudai kwamba Katambi hakuwa mkubwa kuliko Chama chao.
Akizungumza masaa machache baada ya Mwenenyekiti wa Baraza hilo kuhamia CHADEMA, Ole Sosopi amesema kwamba Patrobasi hakuwa Bavicha kwani aliingia ndani ya chama hivyo akiwa hana umaarufu hivyo kuondoka kwake kusiwavunje moyo vijana vingine na kusisitiza kwamba bado baraza hilo la vijana lipo imara.
"Patrobas siyo Bavicha, ila yeye alikuwa sehemu ya Bavicha. Bavicha ipo imara na hii ni taasisi. Na Patrobasi kuondoka Chadema siyo jambo geni, ni jambo la kawaida kama jinsi viongozi wengine wavyotoka chama kimoja kwenda kikingine. Tunamtakia kila la kheri huko alipokwenda. Vijana wetu waendelee kuiwa busy kufanya kampeni kwa ajili ya uchaguzi na wasihangaike na habari za Patrobas". Ole Sosopi
Ameongeza kwamba "Ndani ya Chadema hakuna mtu maarufu isipokuwa Patrobas alipata umaarufu alipokuwa ndani ya Chama na ameondoka, hivyo Chama kitaendelea kuwa imara siyo kwa ajili ya mtu mmoja. Kupitia uchaguzi huu mdogo tunapaswa kutuma meseji kwa CCM na yeye Katambi  hivyo vijana msihamishwe na hili jambo mkaacha kuendeleza kampeni". Ole Sosopi
Aidha aeongeza kwamba kitendo cha Patrobas kuhamia CCM ni usaliti ambao ameudhihirisha kwa watanzania na wanachama kuungana na watu au serikali ambayo imeshindwa kumbaini nani aliyempiga risasi mwanasheria mwenzake Tundu Lissu.
Ameongeza kwamba kinachofanyika na CCM siyo siasa bali ni 'Project' inayofanyika kushawishi watu waone kwamba CCM imebadilika lakini ukweli ni kwamba "CCM ni ileile na madudu yake ni yaleyale kwa zaidi ya mika 50 nawashauri wafanye siasa zinazogusa wananchi"


Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), imesema kuwa agizo la kuhusu kumchunguza aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu imelisikia na imeanza kulifanyia kazi.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Mkurugenzi wa Takukuru, Brigedia Jenerali,  John Mbugo ameitoa leo akizungumza na wanahabari ikiwa ni siku moja baada ya Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamis Kigwangala kumtuhumu Nyalandu  kwa matumizi mabaya ya madaraka.


Brigedia Jenerali,  John Mbungo amesema kuwa endapo wakimkuta Nyalandu na hatia watamfikisha panapostahili.
Dk Kigwangalla  jana bungeni wakati akichangia Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka 207/2018 aliiagiza Takukuru na polisi kumchunguza Nyalandu kwa madai kwamba aliisababishia serikali kukosa mapato na tuhuma zingine zenye kuhusisha rushwa. 
Dk Kigwangala alisema Nyalandu aliikosesha Serikali mapato ya Sh32 bilioni kwa miaka miwili aliyohudumu katika wizara hiyo kwa kushindwa kusaini sheria ya tozo kwa hoteli za kitalii.
Hata hivyo Mh. Nyalandu kupitia mitandao ya kijamiii amekuwa akikanusha tuhuma alizoelekezewa na Waziri Kigwangala na kusema kuwa hizo ni tuhuma zenye lengo la kumchafua pamoja kuwaogopesha watu wengine wenye nia ya kuhama Chama Cha  Mapinduzi.

Mbunge wa Iringa Mjini kwa tiketi ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mchungaji Peter Msigwa amefunguka na kusema kuwa katika Bunge ambalo linatarajiwa kuanza Novemba 7, 2017 anakusudia kupeleka hoja ya kumuondoa Spika wa Bunge, Job Ndugai


Msigwa amesema hayo leo kupitia moja ya mtandao wake wa kijamii na kusema kuwa kwa kuzingatia kanuni ya 137 ya kanuni za kudumu za Bunge atapeleka hoja yake hiyo ya kumuondoa Spika wa Bungue. 
"Ninakusudia kupeleka hoja ya kumuondoa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano Tanzania Mhe. Job Ndungai, kwa kuzingatia Kanuni ya 137 ya kanuni za kudumu za bunge ina complement ibara ya 84 (7) (d) ya Katiba" alisema Msigwa 
Mbunge Peter Msigwa ni kati ya wabunge ambao wamekuwa wakilalamika kuwa Spika wa Bunge, Job Ndugai amekuwa akiendesha bunge kwa shinikizo na upendeleo na kudai kuwa hastahili kuendelea kuongoza kiti hicho. 

Nassari, Lema waanika ushahidi wa rushwa Dhidi ya Madiwani Waliohamia CCM

Image result for joshua nassari na Godbless Lema picha za leo
Mbunge wa Arumeru Mashariki (Chadema), Joshua Nassari ameweka hadharani ushahidi wa rushwa na waliopewa madiwani ambao wamejiuzulu Chadema kwa madai ya kumuunga mkono Rais Magufuli.

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Nassari ambaye ameambatana na Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema walitoa ushahidi huo na kueleza wataukabidhi Takukuru na katika taasisi nyingine.

Katika ushahidi wa video  uliorekodiwa viongozi kadhaa wakiwema Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Alexander Mnyeti pamoja Mkurugenzi Mtendaji wa (H) Meru Christopher Kazeri wamesikika wakiwashawishi madiwani kuhama na baadhi waliahidiwa wangelipwa posho za vikao vyao vilivyobaki hadi 2020 na kukamilishwa miradi yao.

Miongoni mwa makubaliano hayo ni kuwa wapewe fedha na kupata ajira na kukamilishwa miradi yote ya maendeleo waliyoahidi ikiwa ni pamoja na wengine kubadilishiwa makazi pamoja na diwani mmoja kusaidiwa gharama za kufanikisha harusi.

Hata hivyo Mbunge Nassari pamoja na Godbless Lema wameahidi kesho watadfika katika ofisi za TAKUKURU Dar es salaam kwa ajili ya kuukabidhi ushahidi huo wa rushwa kwa Mkurugenzi  Valentino Mlowola

Pamoja na hayo wakati Nassari akiutoa ushahidi huo hadharani leo tayari madiwani 10 wa Chama chake wameshapokelewa ndani ya CCM huku wengie wakiwa wamepinga vikali kuhama chama hicho kwa sababu ya rushwa.

Aidha Nassari amesema ameamua kutoa ushahidi huo sasa kwa sababu alikuwa akiendelea kukusanya ushahidi wa kutosha.

Kambi ya jeshi yashambuliwa na Al shabaab nchini Somalia

Image result for al shabaab somalia

Taarifa kutoka Somalia zinasema wanamgambo wa Alshabaab wameishambulia kambi ya jeshi katika mji wa Barire magharibi mwa mji mkuu Mogadishu.
Shambulio hilo limetokea Ijumaa alfajiri na wakaazi wanasema waliamshwa kwa sauti za milipuko miwili mikubwa.
Kundi la Alshabaab limekiri kuhusika na shambulio hilo na limeeleza kwamba liliidhibiti kambi ya jeshi la Somalia na kufanikiwa kuwaua wanajeshi kadhaa.
Hatahivyo maafisa wa serikali katika eneo hilo wamekana tuhuma hizo za Alshabaab, lakini wamekiri kwamba kumekuwa na shambulio.
Wameahidi kutoa taarifa zaidi baadaye.
Kambi hiyo ya jeshi mjini Barire katika eneo la Lower Shabelle ni mojawapo ya kambi zilizo bora na zenye vifaa vya hali ya juu vya kijeshi nchini Somalia.
Katika siku za hivi karibuni kundi la Alshabaab limebadili mtindo wake wa mashambulio kwa kutokabiliana na vikosi vya usalama moja kwa moja, badala yake vimekuwa sasa vikishambulia kambi za jeshi katika maeneo tofuati Somalia.
Wiki kadhaa zilizopita raia 10 waliuawa katika operesheni ya pamoja ya jesh la Somalia na Marekani katika eneo hilo.
Serikali ya Somalia ilidai kwamba si raia waliouawa bali ni wapiganaji wa Alshabaab, lakini baadaye ilibadili kauli na kuthibitisha kwamba ni wakulima na iliahidi kulipa fidia.

Mwanamume akamatwa akiwa ameficha dhahabu sehemu ya choo cha nyuma

A Sri Lankan customs official displays the seized gold at Colombo airport.
Mamlaka nchini Sri Lanka zimemkamata mwanamume ambaye alijaribu kusafirisha dhahabu na vito vya karibu kilo moja, alivyokwa ameficha sehemu ya choo cha nyuma.
Maafisa wa forodha walipata gramu 904 za dhahabu yenye thamani ya dola 29,370 ndani sehemu ya choo cha nyuma.Mwanamume huyo raia wa Sri Lanka mwenye umri wa miaka 45, alikuwa safarini kwenda nchini India, lakini akasimamishwa kwenye uwanja wa kimataifa wa Colombo.


                       
                                TETEMEKO LA ARDHI LAIKUMBA MEXICO

Jumba Mexico City, 19 September
Juhudi za kuwatafuta waliofukiwa na kifusi kufuatia Tetemeko kubwa la ardhi lililoikumba Mexico zinaendelea licha ya matumaini madogo, kuwakuta hai.
Wafanyakazi wa majanga ya dharura na wale wa kujitolewa wamekuwa wakichimbua vifusi kwa kutumia mikono. Watu 225 wamefariki nchi nzima kutokana na tetemeko hilo, wakiwemo watoto 21, ambao walikufa wakiwa shuleni Mexico city.
Kuna hofu ya watoto zaidi kufariki kutokana na kwamba walikuwa darasani jengo lilipo poromoka.
Rais wa Mexico Enrique Pena Nieto amesema kila dakika inahesabika katika kuokoa maisha ya watu.
Watu 52 tayari wameokolewa kutoka katika kufusi katika mji mkuu wa nchi hiyo.
Tetemeko hilo la ardhi ni la pili kuikumba nchi hiyo katika kipindi cha mwezi mmoja.

0 comments:

Post a Comment

Search This Blog

  • ()
Powered by Blogger.

Yaliyojiri leo

Tanzania yaanza majaribio dawa kinga ya Ukimwi

LIKE OUR FACEBOOK PAGE

Contact us

Name

Email *

Message *