Zimbabwe


Mnangagwa aliyeapishwa Ijumaa kuchukua nafasi ya Robert Mugabe aliyejiuzulu chini ya shinikizo la jeshi na wananchi amemrejesha Patrick Chinamasa kwenye wizara ya fedha na Simbarashe Mumbengegwi katika wizara ya mambo ya nje.

Hatua hiyo imefikiwa wakati Wazimbabwe wakisubiri kwa shauku kubwa orodha mpya ya baraza la mawaziri wakitaka kuona kama atateua sura mpya au ataendelea na waliokuwa watiifu kwa mtangulizi wake.

Gumzo jingine ni ikiwa Mnangagwa atajumuisha baadhi ya wapinzani kusaidia kujenga na kuimarisha uchumi ulioharibiwa.

Chinamasa na Mumbengegwi walikuwa wanasimamia wizara hizo kabla ya kushushwa katika mabadiliko yaliyofanywa na Mugabe mwezi uliopita. Katika mabadiliko hayo ambayo yaliwasukuma nje washirika wa Mnangagwa ndiyo yaliyochangia kuhitimisha utawala wa miaka 37 wa Mugabe wiki iliyopita.

Taarifa ya Katibu wa Baraza la Mawaziri Misheck Sibanda Jumatatu ilithibitisha kuteuliwa kwa Chinamasa na Mumbengegwi.

"Rais ...amevunja baraza la mawaziri, na kwa sasa yuko katika mchakato wa kuunda timu mpya ya mawaziri,” alisema Sibanda. Aliongeza kwamba Chinamasa na Mumbengegwi tayari wameshateuliwa kuwa kaimu mawaziri ili "zisivurugike huduma muhimu kwenye wizara husika".

Zimbabwe kushuhudia demokrasia mpya

Image result for Zimbabwe Emmerson Mnangagwa pictures
Kiongozi mpya wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa amesema nchi yake kwa mara ya kwanza inashuhudia mwanzo wa demokrasia mpya.
Mnangagwa, ambaye anatarajia kuapishwa kushika wadhfa wa Urais wa nchi hiyo siku ya Ijumaa, amesema kipaumbele chake ni kujenga upya uchumi wa nchi hiyo na kuunda ajira mpya kwa idadi ubwa ya watu wasio na ajira.
Katika hotuba yake hiyo, aliyokolezwa na maneno yaliyokuwa yakitumika wakati wa vita vya uhuru wa nchi hiyo, Bwana Mnangagwa alilishukuru jeshi la nchi hiyo, ambalo liliingilia kati baada ya yeye kufukuzwa na Rais Robert Mugabe na kuweza kufanikisha hali iliyopo sasa kwa amani.
Makamu huyo wa Rais wa zamani anayesubiri kuapishwa kuwa Rais wa nchi hiyo alirejea nchini Zimbabwe mapema jana.
Aidha alifahamisha kuwa aliikimbia nchi hiyo baada ya kutishiwa maisha yake baada ya kufukuzwa katika nafasi yake hiyo.

CHINA YAMPONGEZA MGABE

China imesema kuwa imeheshimu uamuzi wa rais Robert Mugabe wa kujiuzulu na kwamba bado atasalia kuwa rafiki wa raia wa Uchina.
Msemaji wa wizara ya maswala ya kigeni Lu Kang ameongezea kuwa sera za China kwa Zimbabwe hazitabadilika. Uhusiano wa China na Zimbabwe ni mkubwa tangu vita vya Rodesian vya msituni.
Bwana Mugabe alikosa kuungwa mkono na Usovieti hivyobasi akarudi China ambayo iliwapatia wapiganaji wake wa Gorila vifaa pamoja na mazoezi.
Mataifa yote mawili yaliimarisha uhusiano wao wa kidiplomasia wakati wa uhuru wa Zimbabwe 1980 na rais Mugabe alimtembelea waziri mkuu wa China mwaka uliofuata.


AU: Hatua ya jeshi la Zimbabwe ni kama mapinduzi

Hatua ya jeshi la Zimbabwe ya kuchukua madaraka na kumzuilia Rais Robert Mugabe, inaonekana kama mapinduzi ya kijeshi, Muungano wa Afrika AU umesema.
Mkuu wake, Alpha Conde, alisema kuwa AU inataka kurejea mara moja hali ya kawaida.
Jeshi linakana kufanya mapinduzi ya kijeshi, na kusema kuwa Mugabe yuko salama, na kuwa hatua zao ni dhidi ya waalifu wanaomzunguka.
Hatua ya jeshi inafuatia mvutano kuhusu ni nani atamrithi Bw. Mugabe.
Makamu wa rais, Emmerson Mnangagwa alifutwa kazi wiki iliyopita, na kuchangia mke wa rais Grace kuwa na fursa wa kumrithi Mugabe, hali iliyosababisha maafisa wa vyeo vya juu jeshini kuhisi kutengwa.
Bwana Mugabe 93, ametawala siasa za nchi tangu ipate uhuru kutoka Uinghereza mwaka 1980.
Akijibu yale yaliyotokea Bw. Conde ambaye pia ni rais wa Guinea, alisema kuwa wanajeshi wa Zimbabwe walikuwa wamejaribu kuchukua madaraka.
Bw. Conde amesema kuwa Misri ilifukuzwa kutoka AU wakati wa mapinduzi ya kijeshi ya mwaka 2013, kwa hivyo jeshi la Zimbabwe linaweza kuwa linajaribu kuzuia hali kama hiyo kw kutaja hatua yao kuwa isiyo mapinduzi ya kijeshi.

Rais Mugabe ataka hukumu ya kifo kuanza kutekelezwa Zimbabwe

Image result for zimbabwe president images for suicide lawRais wa Zimbabwe Robert Mugabe ametaka hukumu ya kifo kurejeshwa nchini humo.
Matamshi yake yanakuja baada ya afisa wa wizara ya sheria, kufichua mwezi uliopita kuwa zaidi ya watu 50 washahukumiwa kifo.
Hukumu ya kifo ilitekelezwa mwisho nchini Zimbabwe mwaka 2005, wakati mtu ambaye alikuwa akiitekeleza kustaafu kwa mujibu wa shirika la AFP.

Akiongea wakati wa maziko ya mwandani wake wa siasa kwenye mji mkuu Harare, Mugabe alisema;
"Wacha turejeshe hukumu ya kifo, watu wanacheza na kifo kwa kuuana. Tunataka nchi iwe na amani na yenye furaha na sio nchi ambapo watu wanuana."
Zaidi ya wafungwa wamehukumiwa kifo, kwa mjibu wa ripoti za AP.

Korea Kaskazini yaionya Australia kutoshirikiana na Marekani

Serikali ya Australia imesema kuwa imepokea stakhabadhi kutoka Korea Kaskazini ikiitaka Canbera kutojihusisha na utawala wa rais Trump.
Barua hiyo imeshutumu onyo la Marekani kwamba itaiangamiza Korea Kaskazini iwapo italazimika kujilinda.
Waziri mkuu wa Australia PM Malcolm Turnbull amesema kuwa barua hiyo pia ilimwa kwa mataifa mengine.
Amesema inaonyesha kuwa shinikizo za kidiplomasia dhidi ya Korea Kaskzini zimeanza kufanya kazi, licha ya barua hiyo kuwa na ufyozi na malalamishi ya kawaida ya taifa hilo.
Barua hiyo yenye ukurasa mmoja ilitumwa kupitia ubalozi wa Korea Kaskazini nchini Indonesia na inadaiwa kutoka kwa kamati ya maswala ya kigeni ya Korea Kaskazini.
Imezitaka serikali nyengine kujitenga na hatua zisizokuwa na heshima za rais Trump ikisisitiza kuwa Marekani inaweza kusababisha janga kubwa la kinyuklia.
Bwana Turnbull amesema kuwa Korea Kaskazini ndio inayosababisha wasiwasi kwa kutishia kuyashambulia mataifa ya Japan, Korea Kusini na Marekani kwa kutumia silaha za kinyuklia.
''Wametuma barua hizi kwa mataifa mengi , kama barua iliosambazwa'', alisema Bwana Turnbull kwa kituo kimoja cha redio 3AW.
Waziri wa maswala ya kigeni Julie Bishop aliitaja barua hiyo kuwa hatua isiokuwa ya kawaida ya Korea Kaskazini
Baadaye bwana Turnbull alionekana kutojali umuhimu wake akiifananisha na ufyozi na malalamishi kuhusu Donald Trump unaotolewa na Korea Kaskazini.
Hatahivyo wote wanakubaliana kwamba huenda ni ishara kwamba shinikizo za kimataifa dhidi ya taifa hilo zimeanza kuzaa matunda na kuwa na matumaini kwamba kutakuwa na majadiliana ya kimataifa.
Siku ya Jumamosi Pyonyang iliionya Australia kwamba haitaweza kuzuia janga iwapo itashirikiana na sera za Marekani dhidi ya utawala wa Kim Jong Un.
Korea Kaskazini imekiuka makubaliano ya kimataifa katika miezi ya hivi karibuni kupitia kufanyia majaribio kombora lake la kinyuklia mbali na kurusha makombora mawili juu ya anga ya taifa la Japan.
Marekani imejibu kwa vitisho vya kijeshi , lakini waziri wa maswala ya kigeni wa Marekani Rex Tillerson anasisitiza kuwa bwana Trump yuko tayari kuutatua mgogoro huo kupitia diplomasia.

Trump aomba ufadhili wa ujenzi wa ukuta na kufukuzwa kwa wahamiaji

Image result for dreamers trump

Ikulu ya Marekani imejumuisha makubaliano yoyote mapya kuhusu wahamiaji wadogo wasio na vibali vya uhamiaji na kuwazuia wahamiaji wasio halali, pamoja na ujenzi wa ukuta mpya kati ya mpaka wake Mexico.
Rais wa Marekani Donald Trump anaomba ufadhili kwa ujenzi wa ukuta, kufukuzwa haraka watu kutoka Marekani na kuajiriwa maelfu ya maafisa wapya wa uhamiaji.
Mwezi uliopita alifuta mpango wa Obama uliofahamika kama "Dreamer" ambao ulikuwa unawalinda wahamiaji 690,000.
Lakini wanademokrat wenye ushawishi katika bunge wamekataa mapendekezo hayo mapya.
Mwezi uliopita Bw. Trump aliliambia bunge la Congress lililo na warepublican wengi kuwa lina miezi sita kukubaliana kuhusu sheria ya kuwasaidia Dreamers.

Dreamers ni akina nani?

Hawa ni vijana ambao walipelekwa nchini Marekani kinyume cha sheria kama watoto na hivyo wanakabiliwa na hatua ya kufuzwa kutoka nchini humo.
Chini ya sera za Obama, vijana hao walikuwa na uwezo wa kuomba vibali vya kufanya kazi na kusoma, lakini wakosoaji wanasema kuwa mpango huo ni sawa na kuwapa kinga wahamiaji haramu.
Tangu mpango huo uanze kutekelezwa karibu hali ya wahamiaji 100,000 imebadilika kati ya karibu wahamiaji 690,000.

Marekani na China kuijadili Korea                                        Kaskazini

Related image
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Rex Tillerson yuko mjini Beijing kufanya mazungumzo na viongozi wa China.
Ajenda kuu katika mkutano huo ni mzozo katika rasi ya Korea.
Marekani na Korea Kaskazini zimekuwa zikirushiana cheche za maneno katika miezi ya hivi karibuni
Utawala wa Trump unaamini China ina umuhimu mkubwa, katika juhudi za kuishurutisha Korea Kaskazini kusitisha uundaji wa silaha zake za Nuklia
China imeonyesha kujitolea kwake katika utekelezaji wa vikwazo vya Umoja wa mataifa dhidi ya taifa hilo.
Siku ya Alhamisi, Beijing ilitangaza kuwa mashirika ya Korea Kaskazini yanayoshirikiana na China hayana budi kufungwa.
Ziara ya Tillerson inakuja huku Rais Trump akitarajiwa kutembelea taifa hilo baadaye mwezi Novemba.

0 comments:

Post a Comment

Search This Blog

  • ()
Powered by Blogger.

Yaliyojiri leo

Tanzania yaanza majaribio dawa kinga ya Ukimwi

LIKE OUR FACEBOOK PAGE

Contact us

Name

Email *

Message *