Wanariadha watano wa Urusi wafungiwa maisha
Wanariadha wengine watano wa Urusi wamefungiwa kushiriki michuano ya kimataifa ya Olimpiki kwa maisha yao yote baada ya kamati ya kimataifa ya Olimpiki kuwabaini kutumia dawa zilizokataliwa michezoni.
Sergei Chudinov, Aleksei Negodailo, Dmitry Trunenkov, Yana Romanova na Olga Vilukhina ndio waliokumbwa na adhabu hiyo.
IOC inasema kufungiwa huko kunatokana na kamati ya 2016 ya McLaren iliyoonyesha watumiaji wa dawa hizo.
Siku ya Jumatatu IOC ilitangaza adhabu hiyo na kuonya kuwa bado itaendelea kwa wale wote watakaojaribu kutumia dawa hizo.
Yannick Bollasie wa Everton arudi katika mazoezi
Mshambuliaji wa Everton Yannick Bolasie amerudi katika mazoezi baada ya miezi 11 akiuguza jeraha.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 alipata jeraha baya wakati klabu yake ilipotoka sare ya 1-1 dhidi ya Manchester United mnamo mwezi Disemba 4, 2016 na hadi kufikia sasa amefanyiwa upasuaji mara mbili.
Raia huyo wa DR Congo alifanya mazoezi na timu ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 23 wiki iliopita kabla ya kujiunga na kikosi kikuu siku ya Jumatano.
Klabu hiyo imesema kuwa alipokea pongezi kutoka kwa wachezaji wenza baada ya kurudi.
Bolasie ameichezea klabu hiyo mara 15 tangu ahamie kutoka Crystal palace 2016.
Italia yashindwa kufuzu kombe la dunia 2018

Mabingwa mara nne wa kombe la dunia Italia, wameshindwa kufuzu fainali za mwa 2018 nchini Urusi ikiwa ni mara ya kwanza tokea mwaka 1958 baada ya kutoka suluhu ya bila kufungana na Sweden.
Hii ina maana kwamba Azzurri watayakosa mashindano hayo kwa mara ya pili tokea kuanzishwa, mara ya kwanza ilikua mwaka 1930.
Kiungo Jakob Johansson wa Sweden aliyefunga goli katika mzunguko wa kwanza alikuwa katika kiwango bora na kuwadhibiti vyema Italia katika uwanja wa San Siro.
Wengi walitaraji Italia kushinda mchezo huu kwa sababu lukuki ikiwemo historia sambamba na kucheza nyumbani.
Italia walitawala mchezo kwa asilimia 75 na kupiga mashuti 27 lakini bahati haikuwa upande wao.
Nusura mshambuliaji Stephan El Shaarawy aandike bao lakini juhudi za mlinda mlango wa Sweden Robin Olsen zilizima ndoto yake.
Matokeo haya yanaifanya Sweden kushiriki mashindano haya tokea mwaka 2006 waliposhiriki kwa mara ya mwisho.
Cristiano Ronaldo atuzwa kuwa mchezaji bora wa kiume 2017

Cristiano Ronaldo ameshinda taji la shirikisho la soka duniani FIFA la mchezaji bora wa kiume wa kandanda mwaka huu kwa mara ya pili mtawalia.
Mchezaji huyo kutoka Ureno, amefunga mabao 44 katika mechi 48 alizoshiriki katika mwaka, kuiwakilisha nchi yake pamoja na timu anayoichezea ya Real Madrid aliochangia kufanikisha ushindi wake katika mataji ya ligi ya Uhispania La Liga na Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Alipokea tuzo yake mjini London na aliwashukuru mashabiki wake wa Real Madrid, wachezaji wenzake, kocha na rais wake.
Antonio Conte apuuzilia mbali taarifa za mtafaruku Chelsea

Meneja wa klabu ya Chelsea Antonio Conte amepuuzilia mbali madai kwamba kuna mtafaruku katika klabu hiyo kutokana na mfumo wake wa mazoezi.
Taarifa zimekuwa zikisema wachezaji wa klabu hiyo wamechoshwa na mazoezi makali wanayolazimishwa kuyafanya na Conte.
Hata hivyo, Mwitaliano huyo amesema mazoezi anayowafanyisha msimu huu ni "70% chini" ya mazoezi aliyowafanyisha msimu uliopita ambapo walishinda Ligi ya Premia.
"Sina habari kuhusu haya," amesema meneja wa Juventus Conte, alipoulizwa kuhusu uvumi huo kwenye vyombo vya habari.
Chelsea wamecheza mechi tatu bila kushinda hata moja mechi zao za karibuni zaidi.
Walishindwa na Manchester City na Crystal Palace Ligi ya Premia kabla ya kutoka sare 3-3 nyumbani dhidi ya Roma Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya Jumatano.
Jumamosi, Chelsea, ambao wamo alama tisa nyuma ya viongozi Manchester City, watakuwa wenyeji wa Watford. Itakuwa mechi yao ya tatu katika siku saba
Conte anaamini kucheza mechi nyingi - pamoja na kukosa muda wa kujiandaa - vimechangia kudorora kwa uchezaji wao.
"Unapocheza kila siku tatu ni vigumu kufanyia kazi mbinu zako za kiufundi na pia hali ya wachezaji," ameongeza.
"Nafikiri sasa hatuangazii zaidi uchezaji kwa kina."
Shinikizo kwa Conte?
Chelsea hawajashindwa mechi tatu mfululizo Ligi ya Premia tangu wiki za mwanzo wa msimu wa 2015.
Jose Mourinho, aliyekuwa ameshinda taji la ligi 2014-15, alifutwa wiki chache baadaye.
Alipoulizwa iwapo anahisi presha, Conte ameongeza: "Nafikiri kila kocha, kila meneja lazima ahisi presha.
"Ninapokwenda nyumbani kwangu huwa nina furaha kwa sababu najua kila wakati huwa najitoleza kabisa katika kazi yangu kwa klabu hii, mashabiki na wachezaji wangu.
"Lakini mwajua vyema kwamba lolote laweza kutokea katika soka."
Mchezaji wa Arsenal aumia akichezea Ujerumani

Beki wa Arsenal Shkodran Mustafi aliumia kipindi cha kwanza katika mechi ambayo mabingwa watetezi wa Kombe la Dunia Ujerumani walikamilisha rekodi ya asilimia 100 katika Kundi C la kufuzu kwa michuano ya mwaka ujao nchini Urusi kwa kuwalaza Azerbaijan 5-1.
Mustafi alichechemea na kuondoka uwanjani kutokana na kile kilichoonekana kama jeraha la misuli ya paja.
Aliumia muda mfupi kabla ya Ramil Seydaev kufungia Azerbaijan bao la kusawazisha.
Alisaidiwa kuondoka uwanjani na nafasi yake ikajazwa na Matthias Ginter.
Vijana hao wa Joachim Low walizinduka baada ya mapumziko ambapo kiungo wa kati wa Liverpool Emre Can alikuwa miongoni mwa wachezaji waliotikisa wavu.
Ujerumani wameshinda mechi zao zote 10 hatua ya makundi, na kufunga mabao 43.
Ndio timu ya kwanza Ulaya kushinda mechi zote 10 kati ya 10 michuano ya kufuzu baada ya Uhispania ambao mwishowe walishinda 2010.
Kiungo wa kati wa Schalke Leon Goretzka alifunga mabao mawili katika mechi hiyo iliyochezewa Kaiserslautern.
Winga Sandro Wagner anayechezea Hoffenheim naye aliibuka mchezaji wa kwanza kufunga mechi tano mfululizo katika mechi zake za kwanza tano kuchezea taifa tangu Ronald Worm mwaka 1978 alipofunga kwa kichwa.
Beki wa Chelsea Antonio Rudiger alijipatia bao la kichwa naye Can akafunga la mwisho kwa kombora kali hatua 25 kutoka kwenye goli.YANGA KUOMBA MSAADA KWA MASHABIKI
Klabu ya soka ya Yanga imerudi tena kwa wanachama wake mara hii ikiwa ni kuhitaji
ushirikiano kwenye ujenzi wa uwanja wa Kaunda ambao utatumika kwenye mazoezi ya timu hiyo.

Msemaji wa Yanga Dismas Ten amesema Yanga inawaomba wanachama na mashabiki wa klabu hiyo kupeleka vifusi kwenye uwanja huo ili kusaidia zoezi la ujenzi linaloendelea.
“Zoezi la ujenzi wa uwanja wetu linaendelea ambapo tumeanza na hatua ya kumwaga vifusi, wanachama wanaleta na tunaomba wengine wazidi kuleta, mtu yeyote anayejua kifusi kinapatikana wapi anaweza kuleta”, amesema Ten.
Yanga imepanga kuuboresha uwanja wa Kaunda uliopo makao makuu ya klabu hiyo mitaa ya Jangwani na Twiga jijini Dar es salaam kwaajili ya kuutumia kwenye mazoezi na mechi za kirafiki za timu ya wakubwa na vijana.Simba yapanda kileleni ikiifunga Stand United mabao 2-1

Timu ya Simba imezima kelele na vijembe vya mashabiki wa Stand United baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 yaliyofungwa na Shiza Kichuya pamoja na Laudit Mavugo kwenye Uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga leo Jumapili.
Kikosi hicho ambacho kimefanikiwa kuchomoka na pointi tatu muhimu, kimeleta matumaini kwa mashabiki wao baada ya mchezo uliopita kutoka sare ya mabao 2-2 na Mbao FC.
Timu hiyo imepanda kileleni ikiwa imefikisha pointi 11 ambazo zimefikiwa na Azam FC pamoja na Mtibwa huku watani zao Yanga walikwaa kisiki jana baada kutoka suluhu ya 0-0 dhidi ya Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Uhuru jana Jumamosi.
Nahodha wa timu hiyo, Mwanjali alisema wanampongeza kipa wao Aishi Manula kwa kuokoa hatari nyingi, huku akisistiza kuyafanyia kazi upungufu uliyojitokea katika kikosi hicho cha leo.
Hata hivyo aliongeza kuwa awali kikosi hicho kililala jambo ambalo liliwapa nafasi wapinzani wao kufunga bao la kufutia machozi.
Wanawake wa Tanzania kukabiliana na Nigeria

Timu ya soka ya taifa ya wanawake chini ya umri wa miaka 20 ya Nigeria inatarajiwa kutua jijini Dar es salaam leo ijumaa ikiwa na kikosi cha watu 31 .
Timu hiyo inataraji kucheza na Tanzania 'Tanzanite' mchezo wa marudiano kuwania kucheza fainali za Kombe la Dunia 2018 nchini Ufaransa .
Mchezo huo utafanyika Jumapili Oktoba mosi Uwanja wa Chamazi nje ya jiji la Dar es Salaam, Mchezo wa Awali Tanzania ilipoteza kwa kufungwa mabao 3-0 nchini Nigeria.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limewapa fursa mashabiki wengi kuingia uwanjani kuishangilia timu yao ya taifa The Tanzanite.
Pep Guardiola: Tunahisi tutafunga mabao mengi

Beki wa kushoto wa Manchester City Benjamin Mendy hatoshiriki katika mechi ya vilabu bingwa Ulaya dhidi ya Shaktar Donetsk katika uwanja wa Etihad kutokana na jeraha la goti.
Mendy alitolewa nje wakati wa ushindi wa City wa 5-0 dhidi ya Crystal Palace siku ya Jumamosi na anatarajiwa kutibiwa mjini Barcelona na mtaalam.
Kiungo wa kati IIkay Gundogan ana jeraha la goti naye beki Vincent Kompany akiugua jereha la nyonga na wote hawatashiriki.
City iliwafunga Feyenoord 4-0 katika mechi ya ufunguzi na klabu hiyo inaongoza jedwali la ligi ya Uingereza wakiwa wamefunga mabao 27 katika mechi nane kufikia sasa msimu huu.
''Tunapocheza nyumbani tunahisi tutafunga mabao mengi'', alisema mkufunzi wa City Pep Guardiola.
''Ni nafasi ngapi tutatengeza na kufungwa ni sawa na msimu ulioipita.Uthabiti unaweza kushuka''kwa hivyo lazima tutahadhari''.
Mourinho hatachukuliwa hatua zaidi baada ya kutimuliwa uwanjani

Jose Mourinho hatachukuliwa hatua zaidi baada ya kutimuliwa uwanjani wakati wa mechi kati ya Manchester United Siku ya Jumamosi.
Meneja huyo na Manchester United alitumuliwa na refa Craig Pawson, kwa kuingia uwanjani wakati wa mechi ambayo Man U walishida kwa bao 1-0.
Baada ya kupokea ripopti ya refa, shirikisho la kandanda barani Ulaya la FA, liliamua kuwa halitachukua hatua zaidi dhidi yake.
Mourinho alipigwa marufuku mara mbili na shirikisho la FA msimu uliopita.
EVERTON YAMUADHIBU ROONEY

Fedha hizo zitapelekwa kwenye kituo cha watu wenye uhitaji maalum.
Everton ina mradi wa kusaidia watu wasiojiweza na imesema fedha hizo zitasaidia sana.
Rooney mwenye miaka 31 aliomba kusahemewa ili aepuke adhabu hiyo.
Siku ya Jumatatu alihukumiwa kutoendesha gari kwa miaka miwili baada ya kukamatwa Septemba 1 akiwa anaendesha gari huku amelewa.
Atafanya pia kazi za jamii kwa siku mia moja.
0 comments:
Post a Comment