Breaking news: Ndalichako aagiza kujengwa kwa nyumba za walimu


Amesema serikali imedhamiria kuondoa changamoto za makazi ya walimu ili ibaki kazi moja ya kufundisha wanafunzi.Related image

Dar es Salaam. Waziri wa Elimu, Sayansi ,Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako amempa mwezi mmoja Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Watumishi Housing,Fred Msemwa kukamilisha mradi wa ujenzi wa Nyumba za walimu.

Agizo hilo amelitoa leo wakati wa ziara ya Shule tatu zilizopo katika wilaya ya Ilala ikiwemo shule ya Pugu Mvuti pamoja na shule ya sekondari Msongola.

Amesema Serikali imeshatoa Sh 5.6 bilioni kwa ajili ya mradi wa ujenzi huo hivyo lazima mradi huo ukamilike kwa wakati,"Naona nikupe mwezi mmoja kukamilisha hatutaki walimu waendelee kuteseka’’, amesema Ndalichako.

Amesema serikali imedhamiria kuondoa changamoto za makazi ya walimu ili ibaki kazi moja ya kufundisha wanafunzi.

Katika hatua nyingine amewataka wakurugenzi kujenga utaratibu wa kuwasikiliza walimu pindi wanapo pelekewa malalamiko yao.

"Wakurugenzi kuweni na utaratibu huo siyo mnakaa na barua za walimu pasipo kuwajibia kwa muda mrefu mwalimu ajue mrejesho wa majibu yake’’ amesema Ndalichako,

Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA),Graceana Shirima amesema kuna mradi wa nyumba za walimu 30 ambao unafanywa na shule husika kwa usimamizi wa halmashauri husika ambao ulianza shule ya sekondari Msongola

"Dhamira kubwa ya mradi huo ni kuhakikisha walimu wanakuwa na makazi mazuri ya kuishi wasipate shida’’amesema Shirima.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo Fred Msemwa alisema kumekuwa na changamoto kubwa ya kuzifikia shule hizo ikiwemo kutumia usafiri wa punda wakati wa kupeleka vifaa vya ujenzi.

Pia amesema ujenzi wa nyumba hizo unafanyika katika wilaya zote hivyo atahakikisha anatekeleza agizo hilo."Nita hakikisha ninatumia muda huo kukamilisha mradi huo hivyo kwa kuweza kuwasaidia walimu,amesema Msemwa.,
Share:

0 comments:

Post a Comment

Search This Blog

  • ()
Powered by Blogger.

Yaliyojiri leo

Tanzania yaanza majaribio dawa kinga ya Ukimwi

LIKE OUR FACEBOOK PAGE

Contact us

Name

Email *

Message *