Msigwa ampa mambo 7 Nyalandu

Mbunge wa Iringa Mjini kwa tiketi ya (CHADEMA) Peter Msigwa amefunguka na kumpongeza Lazaro Nyalandu na kumwambia kuwa amechukua uamuzi sahihi kuachana na chama hicho na kusema amewaonyesha watanzania mambo saba muhimu. 




Msigwa amesema kitendo cha Nyalandu jana kuamua kuachana na Chama Cha Mapinduzi ni wazi kuwa amethibitisha kuwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) si chama tena bali kimekuwa chini ya dola na hakina uwezo wa kuikosoa serikali tena. Msigwa aliainisha mambo hayo saba kama ifuatavyo
1. Nyalandu umethibitisha kwamba CCM sio Chama Cha siasa tena. CCM iko chini ya miguu ya dola na haina uwezo wa kuikosoa serikali tena 
2. CCM imepoteza mwelekeo wake. Imeshindwa kusimamia uchumi, siasa na uongozi wa nchi
3. Misingi ya nchi yetu imebomolewa chini ya utawala wa CCM na umeitisha mwito wa kila mmoja wetu kuijenga upya misingi ya nchi yetu 
4. Tanzania imekithiri ukiukwaji wa haki za binadamu , dhulma na kutekwa na serikali mhimili wa bunge pamoja mahakama.
5. Watanzania wapate fursa ya kuchagua itikadi wanayoona inafaa na sio kutishiwa na kulazimishwa.
6. Mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi nchini yatapatikana kwa mfumo wa demokrasia na Uhuru wa mawazo.
7. Mwisho umeonesha umuhimu wa kupata Katiba Mpya kwa sasa katika Nchi yetu
Mbali na hilo Mbunge Msigwa alimaliza na kusema kuwa "Kuishi nje ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) inawezekana" .
Share:

Manji kurejea Yanga tena

Mashabiki wa klabu ya soka ya Yanga wamebaki kwenye sintofahamu endapo mwenyekiti wao wa zamani Yusuf Manji amerejea kwenye madaraka yake au la.
Kupitia ukurasa rasmi wa klabu hiyo kwenye mtandao wa Instagram  imewekwa picha yenye utata ikielezea kuanza kuuzwa kwa jarida la klabu hiyo linaloitwa ‘Yanga Magazine’,wakati ukurasa wa pili wa Jarida hilo ukiwa na ujumbe unaoashiria kurejea kwa Manji ndani ya Yanga.
Katika ukurasa huo wa pili wa Jarida hilo yameandikwa maneno haya “SHUJAA AMERUDI SHUJAA YUPO NYUMBANI” huku yakipambwa na picha ya mfanya biashara huyo ambaye alijiuzulu cheo hicho miezi kadhaa iliyopita.
Kama hiyo haitoshi inaonekana kuna Makala ambayo ina maelezo ya maneno hayo japo yametiwa kivuli kiasi kwamba hayawezi kusomeka kwa urahisi. Swali linabaki kuwa Je, kuelekea pambano la watani wa Jadi Yanga na Simba siku ya jumamosi huenda Manji akatangaza kurejea kuiongoza Yanga?
Yanga na Simba zitakutana kwenye mechi ya raundi ya nane siku ya jumamosi kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es salaam. Hadi sasa timu hizo zinalingana pointi kila mmoja akiwa na 15 baada ya mechi saba huku Simba ikiongoza kwa tofauti ya mabao.
Share:

Matokeo Darasa la 7 yatangazwa, shule za serikali chali

Image result for wanafunzi darasa la saba picha
Baraza la Mitihani Taifa NECTA limetangaza matokeo ya kuhitimu elimu ya msingi mwaka 2017, na kusema kuwa ufaulu umeongezeka kwa 2.4% ukilinganisha na ule wa mwaka jana 2016.
Taarifa hiyo imetolewa na Katibu Mtendaji wa wa NECTA Dkt. Charles Msonde, na kusema kuwa watahiniwa 662,035 kati ya 909,950 waliofanya mtihani huo wamefaulu kwa kupata alama 100 na zaidi, kati ya alama 250 ambazo walitakiwa kupata.
Dkt. Msonde ameendelea kusema kwamba kati ya waliofaulu wasichana ni 341 020 ambayo ni sawa na 70.93% na wavulana ni 321, 015, ambao ni sawa na 74.80%, na idadi ya watahiniwa wote waliofaulu ni sawa na asilimia 72.76%.
Katibu Mkuu huyo aliendelea kwa kusema kwamba ufaulu  katika masomo ya Kiswahili, Kingereza na Hisabati umepanda kati ya 4.25% na 10.05% ukilinganisha na mwaka jana, huku masomo ya Sayansi na Maarifa ya Jamii ukishuka kati ya 3.56% na 13.97%.
Sambamba na matokeo hayo pia Dkt. Msonde amezitaja shule bora zilizofanya vizuri kitaifa ambazo ni kama zifuatazo
St. Peters - Kagera,
St, Severine - Kagera,
Alliance – Mwanza
Sir. John – Tanga
Palikas – Shinyanga
Mwanga – Kagera
Hazina - Dar es salaam
St. Anne Marie - Dar es salaam
Rweikiza – Kagera
Martin Luther - Dodoma.
Pia Dkt. Msonde amezitaja shule 10 zilizofanya vibaya kitaifa ambazo ni
Nyahaa – Singida
Bosha - Tanga
Ntalasha – Tabora
Kishangazi – Tanga
Mntamba – Singida
Ikolo – Singida
Kamwala – Songwe
Kibutuka - Lindi
Mkulumanzi – Tanga
Kitwai A – Manyara
Share:

Watu 7 wa familia moja wafariki kwa ajali

Watu 7 wamefariki papo hapo na wengine 14 kujeruhiwa, baada ya gari walilokuwa wakisafiria aina ya Noah kugongwa na lori la mizigo wakitoka kwenye sherehe ya harusi wilayani Hanang mkoani Manyara.
Image result for ajali ya gari aina ya noah kuua familia nzima
Ajali hiyo ambayo imetokea usiku wa Oktoba 14, 2017 imehusisha Noah yenye namba za usajili T 744 DJQ, likiwa limebeba watu wa familia moja, kugongwa na lori aina ya semiteller lenye namba za usajili T449 CDR mali ya kampuni ya Lake Hill Paradise ya Singida, na kuleta majonzi na simanzi kwa ndugu wa marehemu.
Share:

POLISI KENYA WAUA WAANDAMANAJI SAKATA LA UCHAGUZI

Watu wawili wauawa maandamano ya Upinzani Kenya

Image result for maandamano kenya watu kupigwa risasi
Watu wawili wameuawa kwa kupigwa risasi wakati wa maandamano ya muungano wa upinzani katika mji wa Bondo, magharibi mwa Kenya.
Taarisa zinasema wawili hao wamefariki baada ya polisi kuwafyatulia risasi waandamanaji ambao inadaiwa walijaribu kuvamia kituo cha polisi cha Bondo katika kaunti ya Siaya.
Mkuu wa polisi wa eneo hilo John Kiarie amesema kwamba hawezi kukanusha au kuthibitisha vifo hivyo kwani bado hajapokea maelezo ya kina kuhusu tukio hilo.
Muungano wa upinzani National Super Alliance wake waziri mkuu wa zamani Raila Odinga umekuwa ukifanya maandamano kushinikiza mageuzi kwenye Tume ya taifa ya Uchaguzi IEBC kabla ya uchaguzi mpya kufanyika.
Alhamisi, serikali ilipiga marufuku maandamano katika maeneo ya kati ya miji ya Nairobi, Mombasa na Kisumu baada ya visa vya uporaji kushuhudiwa wakati wa maandamano ya awali.
Jijini Nairobi, polisi leo wamekuwa wakishika doria katika barabara kuu kuwazuia waandamanaji kuingia katikati mwa jiji.
Katika baadhi ya maeneo, polisi walitumia mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya au kuwadhibiti waandamanaji.
Katika jiji la Nairobi, kumukuwepo na taarifa za wanahabari kushambuliwa na polisi hao wa kupambana na fujo.
Mahakama ya Juu nchini humo ilifuta matokeo ya uchaguzi wa urais uliofanyika tarehe 8 Agosti ikisema ulijaa kasoro nyingi kiasi kwamba ilikuwa vigumu kubaini nani alishinda kwa njia halali.
Tume ya uchaguzi ilitangaza uchaguzi mpya ungefanyika tarehe 17 Oktoba lakini baadaye ikabadilisha tarehe hiyo hadi 26 Oktoba.
Bw Odinga ambaye alitarajiwa kukabiliana na Rais Uhuru Kenyatta alijiondoa Jumanne akisema mageuzi ambayo yanahitajika bado hayajatekelezwa.
Mahakama Kuu baadaye iliagiza kuongezwa kwa jina la Ekuru Aukot miongoni mwa wawaniaji wa urais hatua iliyoifanya IEBC kutangaza baadaye kwamba wagombea wote wanane watashiriki.
Hali ya utata kuhusu kuandaliwa kwa uchaguzi huo imezidi kwambi Nasa wameendelea kusisitiza kwamba hawatashiriki.

Bw Odinga kwa sasa yuko ziarani Uingereza na amesisitiza kwamba hatatia saini Fomu 24A ambayo tume ya uchaguzi ilisema anafaa kujaza ndipo ajiondoe rasmi kutoka kwa uchaguzi huo.
Pendekezo la IEBC kuhusu fomu hiyo limekosolewa na baadhi ya mawakili wanaosema fomu hiyo inaweza tu kutumiwa iwapo kumefanyika uteuzi wa wagombea jambo ambalo haliwezekani wakati huu kwani uchaguzi ni wa marudio.

Share:

BREAKING NEWS

Mume aingia chumba cha gesti bubu kininja, ajeruhi

Image result for wearing mask images
 Mkazi wa kijiji cha Nyansurura wilayani Serengeti, Paul Chacha (24) amejeruhiwa koromeo kutokana na kile kilichotajwa kuwa ni baada ya kufumaniwa akifanya mapenzi na mke wa mtu kwenye gesti bubu.
Katika tukio hilo mume wa mtu aliingia katika chumba cha gesti hiyo kininja akipitia darini.
Mwanamke anayedaiwa kufumaniwa akiwa na Chacha, Bhoke Simion (36) mkazi wa kijiji cha Tamukeri pia amekatwa kifundo cha mguu. Tukio hilo lilitokea Oktoba 3 na majeruhi hao wamelazwa katika Hospitali Teule ya Nyerere wilayani hapa.
Katibu wa hospitali hiyo, Mbona Kazare alithibitisha kuwapokea majeruhi hao wakiwa katika hali mbaya. “Chacha alikuwa na hali mbaya, hakuwa na fahamu, damu nyingi zikivuja kwenye koromeo, kichwani, usoni, miguuni, mikono na mwanamke amekatwa kifundo cha mguu wa kushoto,” alisema.
Akisimulia mkasa huo Chacha alisema, “ni mambo ya shetani tu, tulikuwa tumelala gesti bubu ghafla mumewe aliingia ndani kupitia darini na kuanza kutushambulia, alianza na mke wake na mwisho akaja kwangu na kunikata kata ili aniue.”
Alisema kabla ya mwanamume huyo kuwashambulia alifunga milango ya kuingia na kutoka hivyo hawakupata msaada wowote kwa watu na alizinduka baada ya siku mbili akajikuta hospitalini.
Kwa upande wake Bhoke alisema, “sijui nani alimwambia mume wangu maana alikuwa ameenda msibani, tukiwa tumelala tulishangaa anaingia toka darini na panga, akanikata kifundo cha mguu, nilipiga kelele kuomba msaada lakini hakuna aliyetokea,” alisema.
Alisema mbali ya kuwashambulia alichukua Sh80,000 alizowakuta nazo na kisha kutokomea.
Ofisa mtendaji wa Kijiji cha Tamukeri, Mang’era Magesa alisema mtuhumiwa hajakamatwa ingawa anaonekana kijijini hapo. Kamanda wa Polisi Wilaya ya Serengeti, Mathew Mgema alisema hana taarifa hizo na kuwa atazifuatilia.     
Share:

Wanafunzi hatarini kukosa nafasi ya kujiunga na Vyuo vikuu

Kaimu Katibu mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) Prof. Eleuther Mwageni ametoa tahadhari kwa wanafunzi wanaoomba kujiunga na vyuo vikuu kwa mwaka wa elimu 2017/2018 kuwa makini ili kuepuka kukosa nafasi.

Image result for Tanzania commission for Universities icon png image
Prof. Mwageni ameyasema hayo leo ikiwa imebaki siku moja kabla ya kufungwa kwa awamu ya pili ya kutuma maombi. Ameeleza namna ambavyo awamu ya kwanza imekuwa na changamoto ambapo takribani waombaji 180,640 walituma maombi.
“Mfumo wa sasa unahitaji muombaji kuwa makini sana kwasababu akicheza tu anapoteza nafasi, mfano ni awamu ya kwanza tulipokea majina 180,640 kutoka vyuoni lakini yalikuwa na makosa mengi watu walijirudia na kukosea majina yao tulipochambua tukapata majina 77,756 ambayo nayo bado yalikuwa na mapungufu ndio mana tulipitisha majina 44,627 na tukatoa muda kwa wengine watume maombi kwa usahihi katika awamu ya pili”, amesema Prof. Mwageni.
Katibu ameongeza kuwa waombaji wazingatie vigezo vya Vyuo na Kozi wanazoomba kulingana na ufaulu wao ili kuepusha kukosa nafasi kwenye vyuo wanavyoomba kutokana na alama zao kuwa chini wakati vyuo vina idadi ndogo ya wanafunzi huku wanafunzi waliofaulu vizuri wakiwa ni wengi.
Aidha Katibu amewataka waombaji waliochaguliwa kwenye vyuo zaidi ya kimoja kuthibitisha chuo kimoja ndani ya muda uliotolewa na endapo hawatafanya hivyo basi watapoteza sifa za kujiunga na elimu ya juu.
Amewaasa waombaji kutumia vizuri fursa hii ya awamu ya pili kwani hakutakuwa  na muda zaidi wa kufanya udahili maana ratiba za masomo kwa mwaka wa elimu 2017/18 zinakaribia kuanza hivyo zoezi la udahili haliwezi kuendelea na endapo mwanafunzi mtarajiwa atakosea basi itabidi kusubiri hadi 2018/19.
Share:

BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI

Rais Magufuli alifanyia mabadiliko baraza lake la mawaziri Tanzania

Related image
Rais Magufuli ametangaza baraza jipya la mawaziri huku kukiwa na mabadiliko kidogo ambapo amewaondoa mawaziri wanne waliokuemo katika baraza la awali.
Akiwa na takriban miaka miwili ya uongozi amesema amefanya mabadiliko hayo kutokana na kuwepo na nafasi za wazi ambazo zinahitajika kujazwa.
Mawaziri walioachwa ni aliyekuwa Waziri wa Mali asili na Utalii, Profesa Jumanne Maghembe na nafasi yake kuchukuliwa na Hamis Kigwangwala aliyekuwa Naibu Waziri Wizara ya Afya.
Mwingine aliyeachwa ni aliyekuwa Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Mhandisi Gerson Lwenge ambaye nafasi yake imechukuliwa na Mbunge wa Katavi, Mhandisi Issack Kamwele aliyekuwa naibu waziri wa wizara hiyo.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Annastazia Wambura ambaye nafasi yake imechukuliwa na Mbunge wa Viti Maalum CCM, Juliana Shonza.
Aliyekuwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Ramo Makani naye ametupwa nje na nafasi yake kuchukuliwa na Mbunge wa Vwawa, Japhet Hasunga.
Hili ndilo baraza jipya la mawaziri kama lilivyotangazwa na rais Magufuli:
  • 1.Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.
I. Waziri - George Huruma Mkuchika
  • 2.Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).
I. Waziri - Selemani Said Jafo
II. Naibu Waziri - Joseph Sinkamba Kandege
III. Naibu Wazri - George Joseph Kakunda
  • 3.Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira.
I. Waziri - January Yusuf Makamba
II. Naibu Waziri - Kangi Alphaxard Lugola
  • 4.Ofisi ya Waziri Mkuu: Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu.
I. Waziri - Jenista Joackim Mhagama
II. Naibu Waziri - Anthony Peter Mavunde (Kazi, Vijana na Ajira)
III. Naibu Waziri - Stella Alex Ikupa (Walemavu)
  • 5.Wizara ya Kilimo.
I. Waziri - Dkt. Charles John Tizeba
II. Naibu Waziri - Dkt. Mary Machuche Mwanjelwa
.6.Wizara ya Mifugo na Uvuvi.
I. Waziri - Luhaga Joelson Mpina
II. Naibu Waziri - Abdallah Hamis Ulega
  • 7.Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
I. Waziri - Prof. Makame Mbarawa Mnyaa
II. Naibu Waziri - Mhandisi Atashasta Justus Nditiye
III. Naibu Waziri - Elias John Kwandikwa
  • 8.Wizara ya Fedha na Mipango.
I. Waziri - Dkt. Philip Isdor Mpango
II. Naibu Waziri - Dkt. Ashatu Kijaji
  • 9.Wizara ya Nishati.
I. Waziri - Dkt. Medard Matogoro Kalemani
II. Naibu Waziri - Subira Hamis Mgalu
  • 10. Wizara ya Madini.
I. Waziri - Angellah Kairuki
II. Naibu Waziri - Stanslaus Haroon Nyongo
  • 11. Wizara ya Katiba na Sheria.
I. Waziri - Prof. Palamagamba John Aidan Mwaluko
Kabudi.
  • 12. Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
I. Waziri - Dkt. Augustine Philip Mahiga
II. Naibu Waziri - Dkt. Susan Alphonce Kolimba
  • 13. Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga (JKT).
I. Waziri - Dkt. Hussein Ali Mwinyi
  • 14. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
I. Waziri - Mwigulu Lameck Nchemba
II. Naibu Waziri - Mhandisi Hamad Yusuf Masauni
  • 15. Wizara ya Maliasili na Utalii.
I. Waziri - Dkt. Hamisi Andrea Kigwangalla
II. Naibu Waziri - Josephat Ngailonga Hasunga
  • 16. Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
I. Waziri - William Vangimembe Lukuvi
II. Naibu Waziri - Angelina Sylivester Mabula
  • 17. Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.
I. Waziri - Charles Paul Mwijage
II. Naibu Waziri - Mhandisi Stella Martin Manyanya
  • 18. Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi.
I. Waziri - Prof. Joyce Lazaro Ndalichako
II. Naibu Waziri - William Tate Ole Nasha
  • 19. Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
I. Waziri - Ummy Ally Mwalimu
II. Naibu Waziri - Dkt. Faustine Engelbert Ndugulile
  • 20. Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.
I. Waziri - Dkt. Harrison George Mwakyembe
II. Naibu Waziri - Juliana Daniel Shonza
  • 21. Wizara ya Maji na Umwagiliaji.
I. Waziri - Mhandisi Isack Aloyce Kamwelwe
II. Naibu Waziri - Jumaa Hamidu Aweso
Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amemteua Bw. Stephen Kagaigai kuwa Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kabla ya Uteuzi huo, Bw. Stephen Kagaigai alikuwa Kaimu Karani wa Baraza la Mawaziri.
Bw. Stephen Kagaigai anachukua nafasi ya Dkt. Thomas D. Kashilila ambaye atapangiwa kazi nyingine.
Wateule wote wataapishwa Jumatatu tarehe 09 Oktoba, 2017 saa 3:30 Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Share:

NCHINI HISPANIA MAMBO YAMEKUWA MOTO

Catalonia kutangaza uhuru 'siku chache zijazo'

Catalonia itatangaza uhuru wake kutoka Uhispania siku chache zinazokuja, kiongozi wa eneo hilo amezungumza.

Katika mazungumzo yake ya awali tangu ifanyike kura ya maoni siku ya Jumapili, Carles Puigdemont alisema kuwa serikali yake itachukua hatua mwishoni mwa wiki hii au mwanzoni mwa wiki ijayo.

Kwa upande wake mfalme wa Uhispania Felipe VI, amasema kuwa waandalizi wa kura hiyo walikiuka sheria.

Vilevile amasema kuwa hali ya sasa nchini Uhispania sio nzuri na kutaka kuwepo umoja.

Maelfu ya watu kote eneo la Catalonia wamekuwa wakigoma kupinga ghasa za polisi wa Uhispania wakati wa kura, ambapo takriban watu 900 walijeruhwia.
Image result for catalonia people strike  pictures
Alipoulizwa Carles Puigdemont kuhusu ni kipi atakifanya ikiwa serikali ya Uhispania itaingilia kati na kuchukua udhibiti wa serikali ya Catalonia, Bw Puigdemont alisema kuwa yatakuwa ni makosa ambayo yatabadilisha kila kitu.

Bwana Puigdemont alisema kuwa sasa hakuna mawasiliano kati ya serikali mjini Madrrid na utawala wake.

Alipinga taarifa ya tume ya ulaya ya siku ya Jumatatu kuwa kile kinachoendelea Catalonia ni masuala ya ndania ya Uhispania.
Share:

TAHARUKI CHUO CHA NAIROBI-KENYA

Chuo cha Nairobi chafungwa kwa sababu za kiusalama

Image result for police arresting students of university of nairobi  today
Chuo Kikuu cha Nairobi kimefungwa kwa muda usiojulikana kwa sababu ya kile ambacho viongozi wa chuo hicho wamesema ni haja "kudorora kwa usalama" chuoni humo.
Hatua hiyo imechukuliwa baada ya siku kadha za wasiwasi uliotokana na makabiliano kati ya wanafunzi na polisi wa kukabiliana na fujo ndani ya chuo hicho.
"Wanafunzi wote wametakiwa kuondoka vyumba vyao vya malazi mara moja kabla ya saa tatu asubuhi," taarifa ya seneti ya chuo hicho imesema.
Polisi waliingia chuoni walipokuwa wakikabiliana na wanafunzi waliokuwa wakiandamana kulalamikia kukamatwa na kufunguliwa mashtaka kwa kiongozi wa zamani wa wanafunzi wa chuo hicho Paul Ongili, maarufu kama Babu Owino.
Bw Owino, ambaye kwa sasa ni mbunge wa jimbo la Embakasi Mashariki jijini Nairobi, alikamatwa baada ya kudaiwa kumtukana Rais Uhuru Kenyatta.
Image result for police arresting students of university of nairobi  today
Baadaye alikamatwa tena na kufunguliwa mashtaka mengine ya kumshambulia mpiga kura wakati wa uchaguzi mwezi Agosti.
Aliachiliwa kwa dhamana.
Wanafunzi takriban 26 walijeruhiwa. Video ambazo zimekuwa zikisambazwa mtandaoni zimeonyesha maafisa wa polisi wakiwafurusha wanafunzi kutoka kwa vyumba vya malazi na hata kwenye madarasa.
Mkuu wa polisi Joseph Boinnet amesema kufikia sasa ni vigumu kubaini iwapo video hizo ni za kweli na iwapo wanaoonekana wakipigwa na maafisa wa polisi ni wanafunzi.

Mamlaka inayosimamia utendakazi wa polisi na kutetea haki za raia (IPOA) imetoa wito kwa wanafunzi 26 ambao walijeruhiwa kuandikisha taarifa.
"Kuandikishwa kwa taarifa hizi kutatusaidia kuharakisha uchunguzi," taarifa ya IPOA iliyotiwa saini na afisa mkuu mtendaji Dkt Joel Mabonga imesema.
Awali, taarifa ya mwenyekiti wa IPOA Macharia Njeru ilikuwa imesema: "Ni kweli wapo wanafunzi ambao walijeruhiwa na baadhi ya maafisa wa polisi walipokuwa wanakabiliana na waandamanaji. Kufikia sasa, hatujapokea ushahidi wowote wa kuonesha kunaye aliyefariki."
Bw Njeru alisema baada ya uchunguzi, wamebaini nyingi za video na picha ambazo zinaenezwa mtandaoni zikidaiwa kuwaonesha polisi wakiwashambulia wanafunzi ni za uzushi.
Share:

Search This Blog

  • ()
Powered by Blogger.

Yaliyojiri leo

Tanzania yaanza majaribio dawa kinga ya Ukimwi

LIKE OUR FACEBOOK PAGE

Contact us

Name

Email *

Message *