BREAKING NEWS!! FORM FOUR RESULTS OUT!!!!




By Eliud Adson.

Dar es Salaam. Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) limetangaza matokeo ya kidato nne ambapo ufaulu umeongezeka kwa asilimia saba.

Jumla ya watahiniwa 385, 767 walisailiwa kufanya mtihani kidato cha nne mwaka 2017, kati yao 287,713 sawa na asilimia 77.09 ndio wamefaulu ambapo wasichana ni 143,728 sawa na asilimia 75.21 na wavulana 143,985 sawa na asilimia 79.06.

Akitangaza matokeo hayo leo Januari 30, 2018 Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde amesema mwaka 2016 watahiniwa waliofaulu walikuwa 277,283 sawa na asilimia 70.09.

Amesema matokeo ya watahiniwa 50 wa shule ambao walipata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya baadhi ya masomo ya mitihani hiyo, watapata fursa hiyo mwaka huu.
"Watahiniwa 77 wa shule ambao walipata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya mtihani watapata fursa mwaka 2018," amesema Dk Msonde.

Dk Msonde amesema watahiniwa 265 waliobainika kufanya udanganyifu katika mitihani matokeo yao yamefutwa huku mtahiniwa mmoja akiandika matusi katika karatasi yake ya majibu.

BONYEZA HAPA KUYAPATA MATOKEO
Share:

ELIZAYO HB KAJA KIVINGINE ANAKWAMBIA BYE BYE, PAKUA HAPA KUUPATA WIMBO WAKE MPYA

New Hit song from Elizayo unique

ELIZAYO UNIQUE_-_BYE BYE_PRODUCED_BY_CHUMA&MR.T TOUCH_FREE_NATION_.mp3 DOWNLOAD
Share:

Chadema mguu nje, ndani uchaguzi Kinondoni, Siha



Dar es Salaam. Chadema, ambayo pamoja na vyama vingine vitano vilisusia uchaguzi mdogo katika majimbo matatu, sasa ipo njiapanda kusimamisha wagombea katika majimbo ya Kinondoni na Siha.

Wakati bado hakijatangaza kubadili msimamo huo, uongozi wa ngazi ya Wilaya ya Kinondoni umeanza kutoa fomu kwa ajili ya mchakato wa kupata mgombea kwa maelezo kuwa umeruhusiwa na uongozi wa juu wa chama hicho kikuu cha upinzani.

Lakini uongozi huo wa juu umesema bado haujafanya uamuzi kuhusu kushiriki uchaguzi katika majimbo hayo uliopangwa kufanyika Februari 17 na msimamo huo unaweza kutolewa wakati wowote, Mwananchi imeambiwa.

Mkurugenzi wa Mambo ya Nje na Itifaki wa Chadema, John Mrema alisema jana kuwa wameunda kamati ndogo inayofanya utafiti kuhusu mchakato huo na kwamba uchukuaji fomu huo bado haujapewa baraka za ngazi za juu.

“Hatuna uamuzi wowote hadi sasa, ingawa ule wa awali wa kutoshiriki bado upo,” alisema Mrema.
“Lakini leo uamuzi utatoka. Bado tupo katika mjadala.”

Majimbo hayo mawili yanarudia uchaguzi baada ya waliokuwa wanayashikilia Maulid Mtulia (CUF, Kinondoni) na Dk Godwin Mollel (Chadema, Siha), kujiuzulu nafasi zao kwa nyakati tofauti na kuhamia CCM mwezi uliopita.

Mtulia alitangaza kujiuzulu ubunge Desemba 2 mwaka jana akisema hakushawishiwa na mtu yeyote, bali amebaini kuwa Serikali ya CCM inafanya kazi kubwa ya kutekeleza ilani yake na inafanya vizuri katika mambo mengi ambayo upinzani uliahidi kuyatekeleza.

Wakati Mrema akisema bado wanajadili ushiriki wa Chadema, uongozi wa Wilaya ya Kinondoni umeshaanza mchakato wa kupata mgombea wa kumrithi Mtulia ambaye mwaka 2015 alisimamishwa na vyama vinne vilivyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kutokana na makubaliano maalumu.

Uongozi huo umesema utasimamisha mgombea atakayepambana na Mtulia aliyepitishwa na CCM kuwania tena kiti hicho.

Mwenyekiti wa Chadema wa Kinondoni, Waziri Muhunzi aliiambia Mwananchi jana kuwa baada ya kutafakari kwa kina na kuona mwenendo katika uchaguzi uliopita wa marudio katika majimbo matatu, wameamua kuanza mchakato wa kumsimamisha mgombea.

“Chadema wilayani Kinondoni, ndio tulioamua kuuomba uongozi wa juu kusimamisha mgombea wa jimbo hili na tuna imani litarudi mikononi mwa Ukawa,” alisema.

“Ingawa jambo hili halikuwa rahisi, nawashukuru viongozi wa juu kwa kutuelewa na kuturuhusu.
“Ugumu ulikuwapo kutokana na msimamo wa viongozi wa juu kuhusu malalamiko yao waliyoyatoa huko nyuma kuhusu uchaguzi wa kata 43. Hata hivyo, uchaguzi wa majimbo matatu tumeona baadhi ya mambo yameanza kufanyiwa kazi ikiwamo polisi kutoingilia.”

Muhunzi alisema uchaguzi huo ni kipimo kwao cha kuangalia yale malalamiko dhidi ya wakuu wa wilaya kuingilia uchaguzi yatajitokeza tena kwa kuwa kwenye uchaguzi wa majimbo matatu uliofanyika hivi karibuni hayakujitokeza.

Alisema tayari wanachama 11 wamejitokeza kuomba nafasi ya kugombea ubunge wa jimbo hilo kati yao ni madiwani wanne.

“Mwisho wa kuchukua barua za kutangaza nia ya kuomba kugombea ni leo saa 10:00 jioni. Baada ya hapo kamati ya utendaji itakutana kwa ajili kutoa utaratibu wa kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa kugombea jimbo hili.

“Thamani ya fomu ni Sh 250,000 ambazo watangaza nia hao watazichukua na kujaza kisha kuzirudisha kwa hatua nyingine zaidi,” alisema Muhunzi.

Muhunzi aliwataja wanachama waliojitokeza kutangaza nia kuwa ni Juma Uloleulole (diwani Kijitonyama), Agrey Nicolaus, Elisante Emmanuel, Moza Ally, Francis Nyerere, Rose Moshi (diwani viti maalumu), Ray Kimbita (diwani Hananasif) na Mustafa Muro (diwani Kinondoni). Boniface Obedi, Shabaan Moyo na David Assey.

Kuhusu Ukawa, Muhunzi alisema endapo CUF upande wa Maalim Seif Sharif Hamad ungemsimamisha mgombea, Chadema ingeheshimu uamuzi huo kama ilivyokuwa katika Uchaguzi Mkuu wa 2015.

“Kutokana na mgogoro unaondelea ndani ya CUF, tumesikia upande ule wa Profesa Ibrahim Lipumba unasimamisha mgombea, hivyo hatuwezi kuwaachia bora ingekuwa Maalim Seif,” alisema Mahunzi.

Katibu wa Chadema Mkoa wa Dar es Salaam, Henry Kilewo alisema kura za maoni zinatarajiwa kufanyika leo na kwamba mchakato wa kukagua ujazaji wa fomu za kuomba ulikamilika jana.
Kwa upande wa Siha, kaimu mwenyekiti wa Chadema wa Kilimanjaro, Joseph Selasini alisema bado wanasubiri maelekezo ya Kamati Kuu ya chama hicho.

Hali kama hiyo ilijitokeza mkoani Singida ambako uongozi wa mkoa ulisimamisha mgombea jimbo la Singida Kaskazini, lakini viongozi wa taifa wakaagiza aliyepitishwa kugombea ajitoe kuheshimu msimamo wa chama hicho.
Share:

HESLB Yatangaza majina ya taasisi 57 zisizopeleka makato ya wanaufaika wa mikopo kwa wakati

MIKOPO-HESLB.png
Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) imeanika majina 57 ya kampuni, shule, vyuo na mashirika ambayo waajiri wake hawawasilishi makato ya wanufaika wa mikopo kwa wakati.

Uanikaji wa majina hayo kupitia tovuti ya HESLB umekuja siku mbili baada ya kutangaza kufanya hivyo Jumatano iliyopita.
Mkurugenzi Msaidizi Urejeshaji Mikopo, Phidelis Joseph alisema kabla ya kuanza kuwasaka wanufaika 119,497 ambao hawajarejesha mikopo yao, wataanika majina yao hadharani.

Miongoni mwa kampuni zilizotajwa ni pamoja na Taasisi ya Tiba ya Mifupa (MOI), Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (Dawasco), Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Shirika la NSSF, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Puma Energy Limited, Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra), Bohari Kuu ya Dawa (MSD) na Shirika la Taifa la Maendeleo (NDC).

Zipo pia shule za sekondari ambazo waajiri wake hawapeleki fedha kwa wakati licha ya kuwakata wafanyakazi wao.

Akifafanua kuhusu muda wa kuwasilisha fedha za makato ya wanufaika, Mkurugenzi Mtendaji wa HESLB, Abdul-Razaq Badru alisema kila mwajiri ana wajibu wa kisheria wa kuwasilisha makato ya wanufaika wa mikopo ya elimu ya juu kwa Bodi ndani ya siku 15 baada ya mwisho wa mwezi.

“Baadhi ya waajiri wamekuwa hawafanyi hivyo na kuilazimisha Bodi ya Mikopo kuanza kuwasaka kwa nguvu.

“Katika msako huu hatutamuacha mtu au mwajiri yeyote anayekiuka sheria iliyoanzisha Bodi,” alisema Badru.

Kaimu Mkurugenzi wa Habariwa HESLB, Omega Ngole alisema kwamba idadi ya wanaokwenda kulipa madeni yao imeongezeka.

Alisema kwa kawaida ofisi zao za kanda zilizopo Arusha, Dodoma, Mwanza na Zanzibar hupokea wadaiwa wapya kati ya 15 hadi 25 kwa siku, lakini kuanzia jana wamepokea zaidi ya 50.

Akizungumzia zaidi kuhusu ofisi za makao makuu, Ngole alisema: “Tunapokea wadaiwa wapya wanaotaka kulipa zaidi ya 300 ambayo haikuwa kawaida, wapo na viongozi ambao majina yao yapo kwenye orodha ya wadaiwa, wamemaliza leo.”

Alisema kwamba wanawashukuru wote kwa kutimiza wajibu wao kwa kuwa fedha hizo zitatumika kwa ajili ya kuwasomesha wahitaji wengine.
Share:

LIONEL MESS KUONDOKA BARCELONA FC

Baba mzazi wa nyota wa Barcelona Lionel Messi, Jorge Messi amesema, taarifa zinazosamba kuwa endapo jimbo la Catalonia litajitenga kutoka Hispania nyota huyo ataachana na klabu hiyo kuwa ni uongo.
Jorge ambaye pia ni wakala wa mfungaji huyo ameyasema hayo kwenye mahojiano na 'Radio Red' ya Argentina na kufafanua kuwa hakuna kipengele kinachotaka Messi aondoke Barcelona endapo Catalonia itajitenga na Hispania
''Taarifa hizo ni za uongo, mkataba mpya wa Messi hauna kipengele hicho, ila tu kuna maelewano yanayotaka pande zote mbili kuzingatia kuwa Barcelona ni timu kubwa na inawachezaji wakubwa kwahiyo inatakiwa kucheza ligi kubwa haijalishi ni ligi gani ila iwe moja ya ligi kubwa'', amesema Jorge.
Messi ambaye pia ni mfungaji bora wa muda wote wa Argentina mwezi Novemba mwaka jana alisaini mkataba mpya wa kusalia Camp Nou mpaka mwaka 2021 huku gharama ya kuuzwa ikiwekwa kuwa ni € 700 milioni ambazo ni takribani shilingi  bilioni 2.
Msimu huu Messi ana mabao 15 kwenye LaLiga, huku Barcelona ikiwa pointi 45, tisa juu ya Atletico Madrid inayoshika nafasi ya pili ikiwa 36.

Share:

Search This Blog

  • ()
Powered by Blogger.

Yaliyojiri leo

Tanzania yaanza majaribio dawa kinga ya Ukimwi

LIKE OUR FACEBOOK PAGE

Contact us

Name

Email *

Message *