Je wewe ni Mwanachuo bado au umehitimu chuo na unampango wakusoma nje ya nchi?Zingatia haya unapotaka kusoma nje


Vijana wengi kama wewe wenye ndoto za kufika mbali kielimu wanatamani kusoma nje ya nchi. Nakubaliana na wanaotamani kusoma nje ya nchi baada ya kumaliza shahada yakwanza.
Image result for wahitimu wa chuo
Faida ya kumaliza shahada ya kwanza hapa nchini ni kuepuka ulazima wa kujifunza lugha ya nchi husika hasa kama nchi hiyo Kiingereza si lugha ya kwanza ya mawasiliano.
Mara nyingi katika nchi ambazo hazitumii lugha ya Kiingereza, hutumia lugha zao kufundishia katika daraja hili, baadhi ya nchi hizo ni Ujerumani, Ufaransa, Sweden, Denmark na China.
Hivyo, mwanafunzi atalazimika kusoma lugha hizo, kufanya mitihani akifaulu ndiyo aendelee na masomo.
Tofauti na wanaokwenda kwa ajili ya kusoma shahada ya pili na ya uzamivu kwa daraja hili zinatumia lugha ya Kiingereza kufundishia.
Ili kuepuka kupoteza muda wa mwaka mmoja au miwili bora kusoma shahada ya kwanza hapa nchini kabla ya kuomba ufadhili.
Kuna mambo kadhaa yanayofaa kuzingatiwa kwa mujibu wa maelezo yatolewayo na vyuo mbalimbali vya nje vinavyotoa ufadhili wa masomo.
Mwanafunzi au mwombaji anapaswa kwanza kutafuta chuo ambacho kulingana na sifa alizonazo atakubaliwa kujiunga nacho.
Kupata chuo kabla ya kutafuta ufadhili ni muhimu ili kumuhakikishia anayekulipia hata kama ni chuo chenyewe kuwa umekidhi vigezo.
Hii itamsaidia mfadhili au chuo husika kufahamu gharama za masomo yako, lakini kwa wanaosomeshwa na wafadhili hili litawasaidia kukulipia kupitia moja kwa moja katika chuo husika, kwa sababu wapo wafadhili hawatoi fedha wanalipia gharama moja kwa moja.
Kabla hujawa na fikra za kuomba ufadhili, hakikisha unasoma kwa bidii na kupata matokeo mazuri, kwa sababu ndiyo kigezo cha kwanza cha kupata ufadhili wa masomo.
Usisahau pia kuwa na weledi wa kujieleza hususani kwa kile unachokwenda kufadhiliwa kusoma, kwa sababu wengine unapoomba ufadhili kuna nyaraka unatakiwa ujaze za kulielezea hilo.
Jambo lingine la msingi ni kuwa na weledi katika kusoma, kuandika na kuzungumza lugha ya Kiingereza.
Kama tulivyosema hapo awali nchi nyingi hutumia lugha hiyo pekee kufundishia, hivyo kama unababaisha babaisha itakupa taabu kwenda sambamba nao.
Ndiyo maana ninasema kwa shahada ya pili na kuendelea itakuwa bora sana wakaomba hizo nafasi kwa sababu watakuwa na muda wa kunoa kimombo cha hata baada ya kumaliza shahada ya kwanza.
Kabla ya kuomba ufadhili huu pia hakikisha unaboresha mawasiliano. Jiandae kikamilifu kwa sababu unaweza kutumiwa maswali au nyaraka za kujaza kupitia barua pepe.
Pia unaweza kutakiwa kufanya mawasiliano ya ana kwa ana, kwa njia ya simu , yaani kwa kifupi usiwe mtu wa kubabaika katika kujieleza.
Unapojaza maombi ya ufadhili lizingatie sana hili. Usikimbilie kumaliza kujaza kila fomu unayopewa. Jaza kila kitu usiche hata kimoja, lakini fanya hivyo kwa usahihi na umakini wa hali ya juu.
Katika hili halihitaji ujanja ujanja wa Bongo, kila kitu unachoulizwa kina manufaa kwako na kwao siku zijazo hivyo jaza kila unapotakiwa kufanya hivyo tena kwa kuelewa ulichoulizwa na siyo vinginevyo.
Hayo ni machache miongoni mwa mengi unayotakiwa kufanya kabla ya kuomba ufadhili wa masomo nje ya nchi, lakini pia unapochagua chuo linganisha gharama wakati mwingine unaweza kupata ufadhili wa nusu gharama.
Ushauri wa kuzingatia usiombe ufadhili katika chuo kimoja.
Kama kuna changamoto jipange jinsi yakukabiliana nazo, kwani ndio mwanzo wa kuwa na ujasiri katika uthubutu.
Share:

Mrembo achomwa kisu sinza jijin Dar es Salaam, kisa chake sasa balaa tupu

Image result for binti kuchomwa kisu
Inasikitisha! Mrembo aitwaye Asha Ramadhan, mkazi wa Sinza kwa Remmy jijini Dar es Salaam, miezi michache iliyopita alijeruhiwa vibaya kwa kisu na rafiki yake, Jennifer Michael katika kisa kinachoshangaza. Kwa mujibu wa Asha, chanzo cha ugomvi uliosababisha tukio hilo, ni friji ambalo Asha alimpa rafiki yake amhifadhie lakini baadaye akaamua kuliweka bond kwa mtu mwingine bila kumweleza mmiliki wa friji hilo.
Share:

Teksi ndege isiokuwa na rubani yazinduliwa Dubai

Ndege hiyo ilitazamwa ikipaa angani na mwanamfalme Hamdan bin Mohammed.
Dubai imefanya jaribio la teksi ya kwanza ya ndege isio na rubani ambayo wanatumaini itatumika kama chombo cha uchukuzi mijini.
Ndege hiyo isio na rubani yenye nafasi ya watu wawili iliruka kwa dakika tano katika pwani ya ghuba.
Ndege hiyo ilitazamwa ikipaa angani na mwanamfalme Hamdan bin Mohammed. 
Dubai ina malengo makubwa ya kuwa mji wa kiteknolojia huku ndege zisizo na rubani na roboti zikihusika pakubwa katika mpango huo.
Ndege hiyo ya teksi ilibuniwa na kampuni ya Ujerumani ya Volocopter na kampuni hiyo imesema inatumai kwamba ndege hiyo itaanza kufanya kazi katika kipindi cha miaka mitano.
''Utumizi wake utahusisha simu aina ya smartophone, programu na kuagiza ndege hiyo kuruka hadi katika eneo unalopania kuelekea'', alisema Afisa mtendaji wa kampuni hiyo Florian Reuter.
Teksi ndege isiokuwa na rubani awali ilifanyiwa majaribio nchini Ujerumani mnamo mwezi Aprili.
Teksi ndege isiokuwa na rubani awali ilifanyiwa majaribio nchini Ujerumani mnamo mwezi Aprili.
Kampuni pinzani ya China eHand ilitarajiwa kuwa ya kwanza kuzindua msafara wa teksi ndege mjini humo lakini mipango yake ikaonekana kuchelewa.
Dubai imejiweka kuwa mji wa kiteknolojia duniani ikiwa na mipango ya magari ya kujiendesha kusimamia robo ya safari zote kufikia 2030.
Noel Sharkey ambaye ni mwanasayansi wa komyuta na ambaye pia ni mtaalam wa roboti katika chuo kikuu cha Sheffield alisema kuwa: Changamoo kuu itakuwa vikwazo visivyoepukika kama vile kukwepa teksi nyengine, majumba marefu, vindege na ndege zisizokuwa na rubani ambazo zinatumika kusafirisha mizigo.

Share:

Korea Kaskazini yadai Marekani imetangaza vita

Image result for north korea recent images
Waziri wa mambo ya nje wa Korea Kaskazini amedai kwamba rais wa Marekani Donald Trump ametangaza vita dhidi ya taifa hilo.
Ri Yong-ho aliwaambia waandishi wa habari kuwa Korea Kaskazini ina haki ya kudungua ndege za vita za Marekani.
Hi ni hata kwa zile ndege zenye hazipo katika anga ya Korea Kaskazini, aliongeza waziri huyo.
"Dunia ni lazima ikumbuke kuwa Marekani ndiyo ilikuwa ya kwanza kutangaza vita," Bwana Ri alisema.
Pande hizo mbili zimekuwa zikitupiana maneno makali.
Licha ya majuma kadhaa ya misukusuko, wataalamu wanasema kuwa hakuna uwezekano wa makabiliano ya moja kwa moja kati ya Marekani na Korea Kaskazini.
Share:

WAWILI WAFARIKI AJARI YA BASI

Watu wawili wamefariki dunia huku wengine zaidi ya arobaini wakiwa wamejeruhiwa kufuatia ajali ya basi aina ya Fuso yenye namba za usajili T 606 CTY ya kampuni ya Kisumapai linalofanya safari zake kati ya Songea, Mbinga na Nyasa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma Gemini Mushi amethibitisha kutoa kwa ajali hiyo na kusema kuwa watu wawili wamefariki hapo hapo huku majeruhi wengine wakiwa wamepelekwa katika hospitali ya Wilaya ya Mbinga kwa matibabu. 
"Gari hiyo ilikuwa inaendeshwa na dereva Ismail Mohamed Nasoro ilianguka na kupoteza maisha ya watu wawili hapo hapo, huku watu 42 wakiwa wamejeruhiwa mpaka sasa jumla ya majeruhi 33 kati yao walipata matibabu na kuhurusiwa na wengine 9 wanaendelea na matibabu katika hospitali ya Wilaya ya Mbinga, Mbuyura" alisema Gemini 
Baadhi ya majeruhi wamedai kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa dereva pamoja na bus hilo kuwa limebeba abiria wengi zaidi kuliko uwezo wake .
Share:

China yaiwekea vikwazo Korea Kaskazini

Image result for china vs north korea
China imeimarisha vikwazo dhidi ya Korea Kaskazini, ambapo imetangaza usitishaji wa ununuzi wa nguo kutoka Korea kaskazini mbali na uuzaji wa mafuta kwa taifa hilo kuanzia leo na baada ya muda fulani.
Hatua hiyo inaambatana na maagizo ya vikwazo yaliyowekwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa siku 11 zilizopita.
Wachanganuzi wanasema kuwa vikwazo hivyo vitaathiri sana raia wa Korea Kaskazini iwapo vitatekelezwa kwenye mpaka kati ya mataifa hayo ambao hauna doria ya kutosha.
Share:

"Serikali haitaki wachunguzi wa nje" - Mbowe

Mwenyekiti wa CHADEMA Mbowe amesema serikali haitaki kuruhusu wachunguzi toka nje kuja kufanya uchunguzi suala la Lissu kushambuliwa kwa risasi na kuongeza kuwa msimamo wao ni vyombo vya nje kufanya uchunguzi kwani hawana imani na vyombo vya ndani.
Image result for mbowe
Freeman Mbowe amesema hayo leo Septemba 22, 2017 wakati akizungumza na waandishi wa habari kutolea ufafanuzi mambo mbalimbali kuhusu sakata la Tundu Lissu na matibabu yake pamoja na kuelezea baadhi ya kauli ambazo zimekuwa zikitoka upande wa serikali.
"Kamati Kuu yetu iliomba uchunguzi wa sakata la Tundu Lissu ufanywe na chombo ambacho pande zote mbili zinaimani nacho, lakini serikali haitaki na jana kwa bahati mbaya sana Jaji Mkuu akatoa kauli kwamba vyombo vya ndani havijashindwa kufanya uchunguzi, sina kusudio la kubishana na Jaji Mkuu lakini kama kiongozi mwandamizi wa CHADEMA nadiriki kusema 'suspect' wetu namba moja kwenye shambulio la Lissu ni vyombo vya ulinzi na usalama hilo nalisema bila kumung'unya maneno" alisema Freeman Mbowe " amesema Freeman Mbowe 
Mbowe ameendelea kufafanua sababu ya wao kuhitaji uchunguzi wa nje na kusema "hadi sisi kudai vyombo huru vya kiuchunguzi ni kutokana na madhira mbalimbali tumeyapata kwa muda mrefu kutokana vyombo vya ndani vya ulinzi na usalama havina msaada katika madhira yanayotupata".
Ameelezea zaidi kwa kusema; "Baada ya uchaguzi Mkuu 2015 Mwenyekiti wetu wa mkoa wa Geita Alphonce Mawazo alishambuliwa mchana kweupe na watu ambao wanajulikana lakini polisi haikuchukua hatua yoyote ya maana, walisema wanachunguza lakini hawakuchunguza maana hakuna aliyepelekwa mahakamani mwaka wa pili sasa toka amefariki, Ben Sanane msaidizi wangu amepotea huu mwaka wa pili hakuna hatua zinachukuliwa na vyombo vyetu" alisema Mbowe 
Kiongozi huyo wa CHADEMA amesema kuwa wameshafanya mawasiliano na vyombo mbalimbali vya kiuchunguzi kutoka Marekani, Ujerumani na kusema wapo tayari kuja kutoa msaada wa kiuchunguzi wa jambo hilo. 
"Hata sasa hivi tumezungumza na vyombo vya kiuchunguzi vya Marekani, Ujerumani vipo tayari kuja kutoa msaada lakini wanataka maombi kutoka serikalini, ruhusuni hao watu waje kufanya uchunguzi watoe ushahidi wao, msibaki kusema ni CHADEMA, sijui wenyewe kwa wenyewe ,ruhusuni watu wenye utalaam wao waje kuleta vielelezo hapa huo ndiyo msimamo wa CHADEMA" alisema Mbowe 
Mbali na hilo Mbowe alimtaka Jaji Mkuu wa Tanzania kutambua kuwa wao wanamuheshimu na kusema mambo ya uchunguzi hausiki nayo 
"Tunaomba Jaji Mkuu asubiri tu ila mambo ya uchunguzi ni mambo ya polisi, Jaji Mkuu wewe muhimili wako ni Mahakama lakini hili suala la uchunguzi waachie polisi tunakuheshimu sana hatutaki kugombana na wewe, ila unapaswa kutambua kuwa tunapoomba uchunguzi kutoka nje ina maana hatuna imani na vyombo vya ndani watu wetu wanapotea, wanapigwa risasi, wanauwawa lakini hatuoni hatua za maana zikifanyika" alisisitiza Mbowe.
Share:

EVERTON YAMUADHIBU ROONEY

Image result for rooney
Klabu ya Everton ya nchini Uingereza imemlima adhabu ya kukatwa..

Klabu ya Everton ya nchini Uingereza imemlima adhabu ya kukatwa mishahara ya wiki mbili mshambuliaji wake Wayne Rooney kufuatia kukutwa na kosa la kuendesha gari akiwa amelewa.
Fedha hizo zitapelekwa kwenye kituo cha watu wenye uhitaji maalum.
Everton ina mradi wa kusaidia watu wasiojiweza na imesema fedha hizo zitasaidia sana.
Rooney mwenye miaka 31 aliomba kusahemewa ili aepuke adhabu hiyo.
Siku ya Jumatatu alihukumiwa kutoendesha gari kwa miaka miwili baada ya kukamatwa Septemba 1 akiwa anaendesha gari huku amelewa.
Atafanya pia kazi za jamii kwa siku mia moja.
Share:

MAKOSA YA TUME YA UCHAGUZI KENYA YAFICHULIWA

Makosa ya tume ya uchaguzi Kenya yafichuliwa.


SUPREME COURT JUDGES
Mahakama ya juu inaendelea kutoa sababu za kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi wa urais nchini Kenya kufuatia hatua ya upinzani kwenda mahakamani kupinga matokeo hayo.


''IEBC INAFAA KUFANYA MAANDALIZI MAPYA''

Jaji mkuu nchini Kenya David Maraga amefanikisha uamuzi wa mahakama kuu kuhusu kufutiliwa mbali kwa matokeo ya urais.


''Mfumo wa uchaguzi nchini Kenya ulitengezwa kuwa rahisi na wenye uhakika''. ''Kati ya tarehe 8 na 11 mwezi Agosti uchaguzi uliofanywa haukuwa hivyo'' alisema.
''Kesi ya kupinga uchaguzi iliopo mbele yetu ilikuwa rahisi kuelewa''.
''Ni wazi kwamba IEBC haikuelewa. IEBC inafaa kurudi katika maandalizi yake'' , jaji Maraga aliongezea.
''Mahakama nyengine pia ingefanya uamuzi kama huu iwapo makosa yaliofanyika katika uchaguzi yatarejelewa'', aliongezea.
Image result for jaji mkuu kenya


''UCHAGUZI HAUKUWA NA UWAZI WALA HAUKUHAHAKIKIWA''

Mahakama ya juu nchini Kenya imesema kuwa ilifutilia mbali uchaguzi wa urais nchini humo kwa sababu haukuwa na uwazi wala ithibati .


Mahakama hiyo imelaumu tume ya uchaguzi ya IEBC na mwenyekiti wake kwa kushindwa kupokea matokeo yote kabla ya kutangaza matokeo ya urais.
Pia imekosoa tume hiyo ya uchaguzi kwa kukaidi amri ya mahakama kufungua sava za kompyuta zake ili zichunguzwe hatua iliofanya mahakama hiyo kukubali madai ya upinzani kwamba mfumo wa kutangaza matokeo ulikuwa umeingiliwa na kutumiwa vibaya.


UAMZI WA MAHAKAMA KUU KENYA UNAUPA MOTISHA UPINZANI

Wakati jaji Mkuu wa Mahakama Kuu ya Kenya David Maraga alipo batilisha matokeo ya uchaguzi wa Kenya alikuwa amesema kuwa alibaini "hitilafu na ukiukaji wa sheria " katika mchakato wa uchaguzi.


Uamuzi wa leo uliainisha madai yote hayo kwa kina. Mahakama imeishutumu Tume huru ya Uchaguzi na Mipaka nchini humo (IEBC) kwa kushindwa kufuata sheria katika utendaji wake.Shutuma hiyo inakuja wakati IEBC ikikabiliwa na mzozo wa imani kwa raia.
Mahakama imeupatia upinzani silaha zaidi ya kushinikiza kufutwa kazi kwa maafisa wa tume ya IEBC na mageuzi katika mifumo uchaguzi kabla ya uchaguzi wa marudio.
Majaji wameafiki hoja ya upinzani kwamba kampuni iliyochapisha karatasi za kupigia kura, kwamba baadhi ya karatasi hizo hazikuwa na ishara za usalama.
Muungano wa upinzani Nasa wanataka IEBC kuitafuta kampuni nyingine ya kuchapisha karatasi za kupigia kura kwa ajili ya uchaguzi wa marudio.
Hii inamaanisha kwamba mwenyekiti wa tume ya uchaguzi IEBC Wafula Chebukati anakabiliwa na shinikizo kubwa ikubadili kikosi chake na kujiandaa kwa ajili ya uchaguzi, suala ambalo linaonekana haliwezekani.
Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake Uhuru Ruto, ambao hawakuficha ukosoaji wao kwa majaji, walijibu pia. Rais alimtaja Jaji Maraga kama muhuni ''mkora'' na akatishia kukabiliana naye baada ya uchaguzi wa marudio.
Bwana Maraga alijibu tisho hilo kwa njia yaisiyo ya woga.
Alisema atatetea utawala wa kisheria licha ya "vitisho".
Wafuasi wa upinzani nchini KenyaWafuasi wa upinzani nchini KenyaWafuasi wa upinzani nchini KenyaWafuasi wa upinzani nchini KenyaWafuasi wa upinzani nchini Kenya
Share:

HOW TO PREPARE YOUR OWN TUTORIAL


 
                                       prepare your own tutorial:  play tutorial
all right received:  2017.                                                                                                                        
  • Video software
  •  
  • TV Tuners & Video Capture
ARTICLES DEBUT VIDEO CAPTURE SOFTWARE
  • Best video editing software play tutorial
  • tutorial is prepared by:  shamir suleman +255-656-848274 Dodoma Tanzania 

Debut Video Capture Software supports the following formats

AVI, WMV, ASF, MPG, 3GP, MP4, MPV and more

Share:

KUFUTWA KWA MATOKEO YA UCHAGUZI KENYA


Image result for uchaguzi kenya 2017 kuahirishwa
Mahakama ya Juu nchini Kenya imefutilia mbali matokeo ya uchaguzi wa urais uliofanyika mapema mwezi uliopita na kuagiza uchaguzi mpya ufanyike katika kipindi cha siku 60.

Majaji wa mahakama hiyo walisema uchaguzi huo ulijaa kasoro nyingi ambazo ziliathiri matokeo hayo. Uamuzi huo wa umeifanya Kenya kuwa nchi ya kwanza Afrika ambapo upinzani umewasilisha kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa urais na wakafanikiwa.

Mgombea urais wa muungano wa upinzani National Super Alliance (Nasa), waziri mkuu wa zamani Raila Odinga, aliyekuwa amewasilisha kesi ya kupinga matokeo yaliyotangazwa na Tume ya Uchaguzi ameutaja uamuzi huo wa mahakama kuwa wa kihistoria.

"Leo ni siku ya kihistoria kwa Kenya na kwa Afrika. Kwa mara ya kwanza, Mahakama imefutilia mbali matokeo ya uchaguzi wa urais," amesema. "Tulisema tangu awali kwamba safari yetu ya Canaan haiwezi kuzuiwa. Siku ya tarehe 8 Agosti tulivuka mto Jordan."

Bw Odinga amesema upinzani hauna imani kwamba tume ya sasa ilivyo inaweza kuandaa uchaguzi huru na wa haki.
Share:

Search This Blog

  • ()
Powered by Blogger.

Yaliyojiri leo

Tanzania yaanza majaribio dawa kinga ya Ukimwi

LIKE OUR FACEBOOK PAGE

Contact us

Name

Email *

Message *