
Waziri wa mambo ya nje wa Korea Kaskazini amedai kwamba rais wa Marekani Donald Trump ametangaza vita dhidi ya taifa hilo.
Ri Yong-ho aliwaambia waandishi wa habari kuwa Korea Kaskazini ina haki ya kudungua ndege za vita za Marekani.
Hi ni hata kwa zile ndege zenye hazipo katika anga ya Korea Kaskazini, aliongeza waziri huyo.
"Dunia ni lazima ikumbuke kuwa Marekani ndiyo ilikuwa ya kwanza kutangaza vita," Bwana Ri alisema.
Pande hizo mbili zimekuwa zikitupiana maneno makali.
Licha ya majuma kadhaa ya misukusuko, wataalamu wanasema kuwa hakuna uwezekano wa makabiliano ya moja kwa moja kati ya Marekani na Korea Kaskazini.
0 comments:
Post a Comment