Makosa ya tume ya uchaguzi Kenya yafichuliwa.

''Mfumo wa uchaguzi nchini Kenya ulitengezwa kuwa rahisi na wenye uhakika''. ''Kati ya tarehe 8 na 11 mwezi Agosti uchaguzi uliofanywa haukuwa hivyo'' alisema.
''Kesi ya kupinga uchaguzi iliopo mbele yetu ilikuwa rahisi kuelewa''.
''Ni wazi kwamba IEBC haikuelewa. IEBC inafaa kurudi katika maandalizi yake'' , jaji Maraga aliongezea.
''Mahakama nyengine pia ingefanya uamuzi kama huu iwapo makosa yaliofanyika katika uchaguzi yatarejelewa'', aliongezea.

Mahakama hiyo imelaumu tume ya uchaguzi ya IEBC na mwenyekiti wake kwa kushindwa kupokea matokeo yote kabla ya kutangaza matokeo ya urais.
Pia imekosoa tume hiyo ya uchaguzi kwa kukaidi amri ya mahakama kufungua sava za kompyuta zake ili zichunguzwe hatua iliofanya mahakama hiyo kukubali madai ya upinzani kwamba mfumo wa kutangaza matokeo ulikuwa umeingiliwa na kutumiwa vibaya.
Uamuzi wa leo uliainisha madai yote hayo kwa kina. Mahakama imeishutumu Tume huru ya Uchaguzi na Mipaka nchini humo (IEBC) kwa kushindwa kufuata sheria katika utendaji wake.Shutuma hiyo inakuja wakati IEBC ikikabiliwa na mzozo wa imani kwa raia.
Mahakama imeupatia upinzani silaha zaidi ya kushinikiza kufutwa kazi kwa maafisa wa tume ya IEBC na mageuzi katika mifumo uchaguzi kabla ya uchaguzi wa marudio.
Majaji wameafiki hoja ya upinzani kwamba kampuni iliyochapisha karatasi za kupigia kura, kwamba baadhi ya karatasi hizo hazikuwa na ishara za usalama.
Muungano wa upinzani Nasa wanataka IEBC kuitafuta kampuni nyingine ya kuchapisha karatasi za kupigia kura kwa ajili ya uchaguzi wa marudio.
Hii inamaanisha kwamba mwenyekiti wa tume ya uchaguzi IEBC Wafula Chebukati anakabiliwa na shinikizo kubwa ikubadili kikosi chake na kujiandaa kwa ajili ya uchaguzi, suala ambalo linaonekana haliwezekani.
Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake Uhuru Ruto, ambao hawakuficha ukosoaji wao kwa majaji, walijibu pia. Rais alimtaja Jaji Maraga kama muhuni ''mkora'' na akatishia kukabiliana naye baada ya uchaguzi wa marudio.
Bwana Maraga alijibu tisho hilo kwa njia yaisiyo ya woga.
Alisema atatetea utawala wa kisheria licha ya "vitisho".

0 comments:
Post a Comment