POLISI KENYA WAUA WAANDAMANAJI SAKATA LA UCHAGUZI

Watu wawili wauawa maandamano ya Upinzani Kenya

Image result for maandamano kenya watu kupigwa risasi
Watu wawili wameuawa kwa kupigwa risasi wakati wa maandamano ya muungano wa upinzani katika mji wa Bondo, magharibi mwa Kenya.
Taarisa zinasema wawili hao wamefariki baada ya polisi kuwafyatulia risasi waandamanaji ambao inadaiwa walijaribu kuvamia kituo cha polisi cha Bondo katika kaunti ya Siaya.
Mkuu wa polisi wa eneo hilo John Kiarie amesema kwamba hawezi kukanusha au kuthibitisha vifo hivyo kwani bado hajapokea maelezo ya kina kuhusu tukio hilo.
Muungano wa upinzani National Super Alliance wake waziri mkuu wa zamani Raila Odinga umekuwa ukifanya maandamano kushinikiza mageuzi kwenye Tume ya taifa ya Uchaguzi IEBC kabla ya uchaguzi mpya kufanyika.
Alhamisi, serikali ilipiga marufuku maandamano katika maeneo ya kati ya miji ya Nairobi, Mombasa na Kisumu baada ya visa vya uporaji kushuhudiwa wakati wa maandamano ya awali.
Jijini Nairobi, polisi leo wamekuwa wakishika doria katika barabara kuu kuwazuia waandamanaji kuingia katikati mwa jiji.
Katika baadhi ya maeneo, polisi walitumia mabomu ya kutoa machozi kuwatawanya au kuwadhibiti waandamanaji.
Katika jiji la Nairobi, kumukuwepo na taarifa za wanahabari kushambuliwa na polisi hao wa kupambana na fujo.
Mahakama ya Juu nchini humo ilifuta matokeo ya uchaguzi wa urais uliofanyika tarehe 8 Agosti ikisema ulijaa kasoro nyingi kiasi kwamba ilikuwa vigumu kubaini nani alishinda kwa njia halali.
Tume ya uchaguzi ilitangaza uchaguzi mpya ungefanyika tarehe 17 Oktoba lakini baadaye ikabadilisha tarehe hiyo hadi 26 Oktoba.
Bw Odinga ambaye alitarajiwa kukabiliana na Rais Uhuru Kenyatta alijiondoa Jumanne akisema mageuzi ambayo yanahitajika bado hayajatekelezwa.
Mahakama Kuu baadaye iliagiza kuongezwa kwa jina la Ekuru Aukot miongoni mwa wawaniaji wa urais hatua iliyoifanya IEBC kutangaza baadaye kwamba wagombea wote wanane watashiriki.
Hali ya utata kuhusu kuandaliwa kwa uchaguzi huo imezidi kwambi Nasa wameendelea kusisitiza kwamba hawatashiriki.

Bw Odinga kwa sasa yuko ziarani Uingereza na amesisitiza kwamba hatatia saini Fomu 24A ambayo tume ya uchaguzi ilisema anafaa kujaza ndipo ajiondoe rasmi kutoka kwa uchaguzi huo.
Pendekezo la IEBC kuhusu fomu hiyo limekosolewa na baadhi ya mawakili wanaosema fomu hiyo inaweza tu kutumiwa iwapo kumefanyika uteuzi wa wagombea jambo ambalo haliwezekani wakati huu kwani uchaguzi ni wa marudio.

Share:

0 comments:

Post a Comment

Search This Blog

  • ()
Powered by Blogger.

Yaliyojiri leo

Tanzania yaanza majaribio dawa kinga ya Ukimwi

LIKE OUR FACEBOOK PAGE

Contact us

Name

Email *

Message *